Polepole amjibu Nyalandu
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amemponda aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akisema walishamweka pembeni kwa kuwa hakuwa mtu wa muhimu kwao. Akizungumza jana Jumatatu usiku katika kipindi cha Msemakweli kinachorushwa na Channel Ten, Polepole aliyekuwa akizungumzia mafanikio ya Rais John Magufuli kwa kipindi cha miaka miwili, alimtakia heri Nyalandu huku pia akisema amejimaliza mwenyewe. “Ameondoka mwanachama mmoja wa CCM leo (jana) amekwenda upinzani. Katiba yetu hii ya Jamhuri ya Muungano inasema kila mtu ana uhuru wa kujiunga na chama chochote. Tunaheshimu uamuzi wake, tunamkatia heri katika chama anakokwenda,” alisema Polepole. “Aliyeondoka leo ni ‘very insignificant’ yaani kwa Kiswahili hatujaona utofauti. Ndiyo maana sisi tumetoa maelekezo kwa Serikali kwamba, watu ambao hawakuweza kutukimbiza katika awamu ya tano kwenye maendeleo ya Taifa letu kwenye uongozi wa awamu ya tano wawekwe benchi kwanza. Sasa wamewekwa benchi,” ...