MBOWE ALEZA MSIMAMO WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA KUTOKUWA NA IMANI NA VYOMBO VYA USALAMA NCHINI
MKT WA CHADEMA FREEMAN MBOWE |
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema gharama za
matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyelazwa katika
Hospitali ya Nairobi nchini Kenya zimefikia Sh412.7 milioni.
Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa
habari mchana wa leo jijini Dar es
Salaam, ambapo amewataka watanzania kuendlea kuchangia gharama za matibabu ya Mbunge huyo.
Aidha mwenyekiti huyo ameelezea msimamo wa chama hicho
kutokuwa na imani na jeshi la polisi nchini kwa kile alicho kieleza kuwa jeshi
hilo halijatoa ufafanuzi wowote kuhusu matukio kadhaa yakiwemo mauaji na
kupotea kwa Ben Saanane aliyekuwa makamo wa Mwenyekiti wa chama hicho
Lissu ambaye ni mwanasheria wa chama hicho, amelazwa
hospitalini hapo tangu Septemba 7 aliposhambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi
akiwa maeneo ya nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.
Comments
Post a Comment