Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.
Zaidi ya wakazi 1000 wa kijiji cha Kabuga katika kata ya Kanoge mkoani Katavi wanakabiliwa na adha ya maji safi na salama.
Baadhi ya Wanawake katika eneo hilo wamewalaumu viongozi wa kijiji hicho kutokana na kushindwa kutatua tatizo hilo, na wengine wamesikika wakisema walipewa ahadi hewa kipindi cha uchaguzi wa 2015.
Baadhi ya Wanawake katika eneo hilo wamewalaumu viongozi wa kijiji hicho kutokana na kushindwa kutatua tatizo hilo, na wengine wamesikika wakisema walipewa ahadi hewa kipindi cha uchaguzi wa 2015.
Miongoni mwao wameeleza kuwa utawala wa serikali ya kijiji hicho, umeingiza udanganyifu hata katika mambo ya msingi kama vile huduma za kijamii.
j
Mwandishi wa habari Alinanuswe Edward akimhoji mkazi wa kijiji cha Kabuga katika kisima cha maji kinachotumika na wakazi wa eneo hilo |
Mwenyekiti wa kijiji hicho Benjamini Ezekiel amekili kuwepo kwa tatizo hilo na kueleza jitihada za serikali kuwa ni kuongeza idadi ya vizima ili viweze kukidhi mahitaji ya wakazi.
Lakini visa vya ugomvi ndani ya familia vinatajwa kukithiri katika kijiji hicho ,wanaume hutajawa kuwa vinara wa kadhia hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwa baadhi ya wanaume wenye misimamo hasi huwa tuhumu wake zao kutumia tatizo la maji kama nyenzo ya kufanikisha usariti wa ndoa zao.
Kijiji hicho kilicho kaskazini mwa mkoa wa Katavi ulio kusini magharibi ya Tanzania kina kisima kimoja tu, jambo ambalo wenyeji hasa wanawake wanadai kutumia muda mwingi kutafuta maji kuliko kufanya kazi za kimaendeleo.
Comments
Post a Comment