SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA



Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi Mh Raphael Kalinga amesema tayari ametoa taarifa kwa katibu mkuu kuarifu kuhusu aliyekuwa diwani wa Kata ya Katumba katika halmashauri hiyo kufungwa miaka mitatu jera kwa kosa la kupokea na kushawishi rushwa.

Akizungumza na Mpanda radio fm mapema leo kupitia kipindi cha Kumekucha Tanzania Karinga amesema halmashauri inajipanga kwenda katika kata hiyo ili kukutana na watendaji ambao wamekuwa hawatoi ushirikiano kwa Diwani wa viti maalumu katika kata hiyo, akieleza kuwa suala hilo lina leta mkwamo wa maendeleo kwa wananchi.

Katika hatua nyingine amesema wanasubiri maelekezo kutoka ngazi za juu kujua hatima ya suala hilo.

Mapema siku ya jana Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Mh Rhoda Kunchela amesema kitendo cha wananchi wa kata hiyo kukosa Diwani hakikubaliki kwani kinadhoofisha jitihada za maendeleo  ya wananchi.

Diwani wa kata hiyo Seneta Baraka alifungwa mwaka jana miaka 3 jera  kwa kosa la kupokea rushwa kwa mfugaji wa kata hiyo ili amuidhinishie eneo la kufugia ambalo limepigwa marufuku na Mahakama.

Comments

Popular posts from this blog

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.