MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI




Baraza la Mitihani Taifa NECTA limetangaza matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2017, na kusema kuwa ufaulu umeongezeka kwa 2.4% ukilinganisha na ule wa mwaka jana 2016.


aarifa hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa wa NECTA Dkt. Charles Msonde, na kusema kuwa watahiniwa 662,035 kati ya 909,950 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata alama 100 na zaidi, kati ya alama 250 ambazo walitakiwa kupata.
Dkt. Msonde ameendelea kusema kwamba kati ya waliofaulu wasichana ni 341 020 ambayo ni sawa na 70.93% na wavulana ni 321, 015, ambao ni sawa na 74.80%, na idadi ya watahiniwa wote waliofaulu ni sawa na asilimia 72.76%.
Katibu Mkuu huyo aliendelea kwa kusema kwamba ufaulu  katika masomo ya Kiswahili, Kingereza na Hisabati umepanda kati ya 4.25% na 10.05% ukilinganisha na mwaka jana, huku masomo ya Sayansi na Maarifa ya Jamii ukishuka kati ya 3.56% na 13.97%.
Sambamba na matokeo hayo pia Dkt. Msonde amezitaja shule bora zilizofanya vizuri kitaifa ambazo ni kama zifuatazo
St. Peters - Kagera,
St, Severine - Kagera,
Alliance – Mwanza
Sir. John – Tanga
Palikas – Shinyanga
Mwanga – Kagera
Hazina - Dar es salaam
St. Anne Marie - Dar es salaam
Rweikiza – Kagera
Martin Luther - Dodoma.
Pia Dkt. Msonde amezitaja shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa ambazo ni
Nyahaa – Singida
Bosha - Tanga
Ntalasha – Tabora
Kishangazi – Tanga
Mntamba – Singida
Ikolo – Singida
Kamwala – Songwe
Kibutuka - Lindi
Mkulumanzi – Tanga
Kitwai A – Manyara

Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.