MADEREVA WA GOMA TANGA
Madereva hao wamegoma kufanya kazi kwa kile kinachodaiwa kupinga uonevu unaofanywa na Askari wa kikosi cha usalama barabarani ambapo wamekuwa wakiwatoza faini na kuwakamata bila makosa.
“Ni kweli madereva wamegoma tangu jana lakini wengine kwenye baadhi ya maeneo wameanza kazi leo na wengine bado wamegoma na tunatarajia kukutana nao asubuhi hii kwaajili ya kuzungumza namna ya kutatua mgomo huo”, amesema RPC Wakulyamba.
Mapema wiki jana RPC Wakulyamba alithibitisha kukamatwa kwa madereva kumi wa mabasi na daladala kwa tuhuma za kuendesha vyombo vyao bila kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani.
Comments
Post a Comment