Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amemfungulia mashtaka ya kudharau Mahakama kiongozi wa Muungano wa Upinani Nchini humo, Nasa, Raila Odinga.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, Rais Kenyatta amefungua mashtaka hayo katika Mahakama ya Juu, ambapo Katibu Mkuu wa chama tawala cha Jubilee, Raphael Tuju, ameushutumu upinzani wa Nasa, kwa kutatiza mafunzo ya maafisa wa uchaguzi kwenye ngome kuu za Odinga magharibi mwa nchi hiyo.
Kesi hiyo ni mfululizo wa hali ya sintofahamu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio wa Urais Oktoba 26.
Upinzani umekuwa ukishinikiza kufanyika kwa mabadiliko ndani ya Tume ya Uchaguzi na Mipaka, hasa ukiwalenga maafisa wa tume hiyo wanaotuhumiwa kuvuruga uchaguzi uliobatilishwa wa Agosti nane mwaka huu.
Comments
Post a Comment