Wakulima mkoani Katavi waitaka serikali ilegeze mashariti ya kibiashara nnje ya nchi
Baadhi
ya Wafanyabiashara wa mazao ya mpunga Mkoani Katavi wameiomba serikali kufungua mipaka ya biashara ili waweze kuuza
mazao katika nchi jirani.
Wakizungumza
na Mpanda Redio Baadhi ya Wafanyabiashara hao wamesema katika kipindi hiki cha
msimu wa kilimo bei za mazao hushuka
hivyo kupelekea kuuza mazao kwa bei ya hasara.
Siku
chache zilizopita wakulima wa mkoa wa Rukwa
wameiomba serikali ya mkoa huo kuitangazia mikoa jirani kwenda kununua
mazao ya nafaka kutokana na kukosa soko .
Mnamo
mwezi juni 26,2017 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim
Majaliwa alipiga marufuku usafirishaji
wa mazao nje ya nchi bila Kibali kutoka serikalini.
Comments
Post a Comment