WATU 150 WAMEUAWA KATAVI KUTOKANA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI




KATAVI
Kamanda wa polisi Mkoa wa katavi Damasi Nyanda ametoa wito kwa wananchi  kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi dhidi ya watuhumiwa wa makosa mbalimbali wakati wanapowakamata.
Kamanda Nyanda ametoa wito huo wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kalovya kata ya Inyonga ambapo amesema suala la kuchoma moto watuhumiwa halikubaliki badala yake watuhumiwa wafikishwe katika vyombo vya sharia.
Amesema zaidi ya watu wapatao 77 wameuawa wilayani Mlele kwa kipindi cha mwaka 2015 huku mpaka kufikia mwaka huu kwa mujibu wa kamanda Nyanda watu wapatao 150 wameuawa kutokana na wananchi kujichukulia sheria mkononi.


Kwa upande wa makosa ya ubakaji,kamanda Nyanda amesema mpaka mwezi Juni mwaka huu makosa 46 ya ubakaji yameripotiwa katika jeshi la polisi huku visa vya watu kujinyonga,kukutwa wamekufa navyo vikionekana kuwa katika hali ya juu.

Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI