Mamlaka ya Udhibiti wa Fedha na Ofisi ya kuchunguza makosa makubwa ya rushwa Nchini Uingereza, zinachunguza ili kubaini iwapo benki za HSBC na Standard Chartered, zinahusika na kashfa ya rushwa ya nchini Afrika Kusini.





Hatua hiyo imekuja baada ya Mbunge mmoja wa nchini humo, Lord Peter Hain, kusema huenda benki hizo bila kujua zilihusika na utakatishaji wa fedha.
Mbunge huyo amedai kuwa, fedha haramu Paundi milioni 400 huenda zilihamishwa na benki hizo na kuhofia kwamba, fedha hizo zinahusika na Rais Jacob Zuma na familia ya kitajiri ya Afrika Kusini ya Gupta.
Lord Hain amemwandikia barua Waziri wa Fedha, Philip Hammond, na kutaja majina ya watu 27 na makampuni ambayo yanahusishwa na kashfa hiyo ya rushwa

Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI