Bila Lissu na CHADEMA, CCM yangu italala



Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Timu ya Simba, Haji Manara ambaye ni mwanachama wa CCM amefunguka na kusema hajawahi kumshabiki Tundu Lissu wala CHADEMA lakini anaamini bila uwepo wake na CHADEMA basi chama chake CCM kitalala.



Haji Manara amesema hayo leo baada ya kuona picha ya kwanza ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akiwa hospitali jijini Nairobi nchini Kenya ambapo anapatiwa matibabu kufuatia kupigwa risasi Septemba 7, 2017 na watu wasiojulikana. 
"Ohhh God,mimi sijawahi kukushabikia wewe wala chama chako ila nakuombea kwa Mungu upone haraka kaka, urudi katika harakati zako nikiamini bila uwepo wenu chama changu kitalala" aliandika Haji Manara kupitia ukurasa wake wa Instgram. 
Mbali na Haji Manara watu wengine wengi wameonyesha kufurahishwa na hali ya Tundu Lissu baada ya kumuona kupitia picha ambazo zimeanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, Mbunge huyo wa Singida Mashariki anatarajiwa kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu ya awamu ya tatu siku za karibuni. 

Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI