MANISPAA YA MPANDA KUANZA KUAJILI WATENDAJI WA KATA WA MUDA
Mkurugenzi
mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu ameagiza kuajiriwa kwa baadhi ya
maafisa kata wa muda katika baadhi ya Kata.
Amesema
hayo katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika jana katika ukumbi wa
Manispaa ya Mpanda alipokuwa akijibu baadhi ya maswali yaliyo ulizwa na
Waheshimiwa madiwani kuhusu tatizo hilo.
Katika
hatua nyingine amezitaja baadhi ya sababu zilizopelekea upungufu wa watendaji
hao kuwa ni baadhi yao kukumbwa na sakata la watumishi wenye vyeti feki.
Baraza
la Madiwani linaendelea leo ambapo Madiwani watawasilisha mapendekezo mbali
mbali ya utekelezwaji wa bajeti katika kata zao.
Comments
Post a Comment