MASOKO MKOANI KATAVI KUKUMBWA NA UBOVU WA MIUNDO MBINU
MPANDA. NA Mdaki Hussein
Wafanyabiashara katika soko
la Mpanda Hoteli Manispaa ya Mpanda Mkoani katavi wameendelea kulalamikia miundo
mbinu mibovu vyoo sokoni hapo.
Mpanda redio imefika na
kuzungumza na Baadhi ya wafanyabiashara sokoni hapo ambo wamesema kwa muda mrefu
wamekuwa wakilalamikia suala hilo hadi sasa hawaoni viongozi wakitekeleza.
Aidha wengine wameskika
wakisema wamekua wakipata ahadi hewa kutoka kwa viongozi juu ya kutatua kero mbalimbali
sokoni hapo kama maji na umeme.
Kwa upande wake Mstaiki
Meya wa manispaa ya Mpanda amewaomba wafanyabiashara hao kuwa wavumilivu kwa
alichokisema wanalifanyia kazi suala hilo.
Masoko mbali mbali
mkoani Katavi yamekumbwa na kadhia ya miundo mbinu dhaifu kiasi cha kupelekea
kukithiri kawa mararamiko hayo.
Comments
Post a Comment