Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Kenya Wafula Chebukati awalaumu wanasiasa
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Kenya Wafula Chebukati amewashutumu wanasiasa nchini humo akisema wanatatiza maandalizi ya uchaguzi wa marudio Alhamisi wiki ijayo.
Bw Chebukati amesema maandalizi ya uchaguzi huo yanaendelea vyema lakini katika mazingira ya sasa ni vigumu kuandaa uchaguzi huru na wa haki iwapo hakutakuwa na mabadiliko.
Mwenyekiti huyo, ameeleza kuwa amejaribu kutekeleza mageuzi mengi kwenye maandalizi ya uchaguzi wa marudio lakini "majaribio yangu yamepingwa (kwa kura) na makamishna wengi."
"Chini ya mazingira haya, ni vigumu kuhakikisha uchaguzi huru na wa kuaminika. Nina uhakika kwamba bila mabadiliko muhimu katika sekretariati huenda tusiwe na uchaguzi huru, wa haki na wa kuaminika," amesema.
inawahimiza wafanyakazi wa tume ambao wametajwa sana (kuhusiana na kasoro za awali) waondoke kwenye nyadhifa zao na kutoa nafasi kwa kundi maalum la kusimamia uchaguzi kufanya kazi bila kuingiliwa."
Bw Chebukati amesema hayo saa chache baada ya mmoja wa makamishna wa wa tume hiyo Dkt Roselyn Akombe kutangaza kujiuzulu akiwa Marekani na kusema hana mipango yoyote ya kurejea Kenya hivi karibuni.
Kiongozi huyo wa tume amesema mashauriano ya kisiasa yanahitajika sana kwa sasa na kutoa wito kwa viongozi wa muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) na chama cha Jubilee kukubali kulegeza misimamo yao na kushauriana.
Comments
Post a Comment