POLE POLE ALIAMUSHA DUDE
KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI CCM HUMPHREY POLEPOLE |
Wakati
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akiwataka wakuu wa wilaya
nchini kuwa na hekima ya kuridhika na vyeo walivyonavyo moto umeendelea kuwaka
ndani ya chama hicho, baadhi ya makada na wachambuzi wa siasa kukosoa pendekezo
lake la wagombea kuwa wakazi wa majimbo husika.
Wiki
iliyopita, Polepole alisema katika kipindi cha redio Times kuwa wanachama
wanaotaka kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM 2020, sasa watalazimika kuwa wakazi
wa eneo wanalotaka kuliwakilisha, sharti ambalo linaweza kuwaondoa takriban
nusu ya wabunge wa sasa.
Tamko hilo
la Polepole lilizua mjadala mzito jambo lililosababisha Katibu wa Halmashauri
Kuu ya Taifa ya CCM Organaizesheni, Pereira Silima alitoa taarifa kueleza kuwa
hakuna mahali popote katika mabadiliko ya katiba yao palipoandikwa kuwa
wagombea wa udiwani na ubunge watajadiliwa kwa sifa ya kuishi jimboni.
Ukiacha
hilo juzi usiku katika kipindi cha ‘Tuambie’ kinachorushwa na televisheni ya
TBC, Polepole alizungumzia suala jingine la kuwa kanuni za uchaguzi
haziwakatazi wakuu wa wilaya kuwa wajumbe wa mkutano mkuu wa Taifa wa CCM,
wanapaswa kuwa na hekima.
Kauli ya
Polepole imekuja wakati tayari kukiwa na wakuu wa wilaya wanne, mkuu wa mkoa na
makatibu tawala walioshinda katika chaguzi za chama hicho zilizofanyika hivi
karibuni.
Walioshinda
ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego ambaye aligombea ujumbe wa
mkutano mkuu wa CCM baada ya kupata kura 311.
Mwingine
ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Nanyumbu, Salum Palango aliyepata kura 295.
Wakuu wa
wilaya walioshinda ni Simon Odunga (Chemba) aliyeshinda kwa kura 432, Christina
Mndeme (Dodoma) na Elizabeth Kitundu (Bahi) wote kutoka mkoani Dodoma.
Mkoani
Morogoro, walioshinda ni Alhaji Mohamed Utaly (Mvomero) na Seriel Nchembe
(Gairo).
Wakuu
wengine wa wilaya walioshinda ni Raymond Mushi (Babati) mkoani Manyara, Herman
Kapufi (Geita), katibu tarafa wa Makuyuni (Arusha), Paul Kiteleki na mkuu wa
Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Alexander Mnyeti.
“Ukienda
kwenye kanuni za uchaguzi za 2017 fungu la 25: Nafasi ya uongozi ni kazi ya
muda wote (inazitaja hapo), Mkutano Mkuu wa Taifa haujatajwa, lakini mkuu wa
wilaya ni kiongozi wetu wa Serikali pia ni kiongozi wetu wa chama,” alisema
Polepole na kuongeza:
Mkuu wa
wilaya ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ni mjumbe wa halmashauri kuu ya
wilaya na ni mjumbe wa mkutano mkuu wa wilaya. Huyu pia ni kamisaa wa Serikali,
‘public officer’ anayefanya kazi zote za chama. Sasa nikasema hekima pale
ituongoze, yaani mtu ujiongeze mwenyewe.”
Aliendelea
kusema: “Kama wewe una dhamana zote hizi, kwa nini mkutano mkuu tusimwachie
mwanachama mwingine asiye na dhama nyingine yeye ashiriki kwenye mkutano wa
chama?”
Polepole
aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma mkoani Mara na baadaye Ubungo jijini
Dar es Salaam alisema kwa sasa kuna wakuu wa wilaya wapatao 166 na kama wote
wataomba nafasi hizo, watafurika kwenye nafasi za chama hicho.
“Kama
wakuu wa wilaya wote watachukua kwa pamoja wako 166, zamani mkutano mkuu
tulikuwa 2400 sasa hivi tumepunguza idadi tumekuwa 1,700, hao ni wanachama
walioomba dhamana halafu kati ya hao 166 ni wakuu wa wilaya,” alisema Polepole
na kuongeza:
“Upande wa
pili ni hekima ya kuwa na kiasi. Wewe una nafasi kadhaa, hizi nafasi nyingine
tumwachie mtu mwingine. Hiyo inakuja kutokana na maelekezo yetu kwenye fungu la
22 kwamba; mtu mmoja kofia moja. Ukiwa kiongozi una dhamana tayari basi hii
nyingine waachie wengine nao waweke mawazo yao katika kupeleka mbele chama chetu.”
Mbunge wa
Nzega Mjini(CCM), Hussein Bashe katika maoni yake alisema dhana ya ukazi
imepitwa na wakati pamoja na kuwa inaenda kinyume na Katiba, kanuni na tamaduni
za chama hicho.
“Nimeisikia
kauli ya katibu wangu nadhani ni kauli ambayo inahitaji mjadala mpana, binafsi
naamini chama chetu kina katiba, Kanuni na maadili. Utamaduni huu ndo msingi a
chama chetu ambao unatuongoza,” alisema.
Bashe
alisema dhana ya aina hiyo ikipewa fursa siku moja itakuja hoja ya kwamba
anayetakiwa kugombea uchaguzi ni lazima awe mchaga, ikiwa hoja ya mkazi itakosa
uhalali na nguvu kisiasa.
“Fursa
aina hii ya mawazo ikipewa uhalali, siku moja hoja ya mkazi ikikosa uhalali na
nguvu ipo siku tutatumia ukabila, ikiisha tutasema udini kwa kuwa ukiwa
muislamu utayajua sana matatizo ya waislamu,” alisema.
Bashe
alisema mbunge anayo majukumu yake nayo ni uwakilishi na kwamba, mbunge kuwa
mkazi haiwezi kumfanya azifahamu shida za watu yapo mambo ya msingi ambayo yanatakiwa
kutazwa.
“Je Mbunge
ametimiza majukumu yake? Ametimiza ahadi zake? Amekuwa muwakilishi mzuri wa
wananchi wake? Dhana hii binafsi naiona kama ni dhana ‘aoutdated’ (imepitwa na
wakati),” alisema.
Alisema
kuwa hoja ya mkazi haimfanyi mtu kuwa mwakilishi mzuri na ifahamike kwamba
wabunge wengi wanafanya shughuli mbalimbali ikiwazo zao binafsi zinazosaidia
maendeleo ya wananchi wake.
“Mwalimu
Nyerere alitengeneza mifumo toka Tanu mpaka CCM ya kumuandaa kiongozi kuanzia
Chipukizi, Yuth Legue.Haya ni maeneo ya majaribo na makosa
Alisisitiza
kuwa zipo nafasi ambazo kiongozi hatakiwi kutoa kuli yenye Taswira ya kuwagawa
watanzania kwa msingi wowote ule hata kama utakuwa na nia njema.
“Tumeona
kauli ya Silima, ni kauli sahihi kabisa. Hivi karibuni kumekuwa na matamko
controversial ambayo unajiuliza duh hivi Katibu Mkuu yupo wapi? Hata kama
tunafanya reform, hii ni njia sahihi? Vitisho vimekuwa vingi sana,”alisema
Bashe.
Alieleza
kuwa CCM ni wanachama na wanachama
“Leo wana
CCM wameanza kuwa wanyonge na hofu ya kukosa ari. Tumeanza kujenga tabaka la
watawala na watawaliwa ndani ya chama, ni muhimu sana kila kiongozi aheshimu
katiba na kupima kauli zetu,”.
Comments
Post a Comment