ZITTO KABWE MIKONONI MWA POLISI KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI



Mbunge huyo wa Kigoma mjini, alikamatwa mara ya kwanza asubuhi ya Jumanne nyumbani kwake mjini Dar es salaam na kupelekwa kituo cha polisi Chang'ombe.
Baada ya masaa kadhaa mbunge huyo aliachiliwa huru kabla ya kukamatwa tena.
Wakili wa Bwana Kabwe, Stephan Ally Mwakibolwa anasema sababu zilizotajwa kwa kushikwa kwake ni kutoa maneno yanayodaiwa kuwa ni ya uchochezi.
"Kauli kubwa haswa wanayosema ni kuihusisha serikali ya CCM na matukio ya watu waliookotwa katika fukwe za bahari ya hindi wakiwa wamefariki ,pamoja na tukio la mbunge Tundu Lissu"
Bwana Kabwe sasa amepelekwa katika kituo cha polisi cha Kamata mjini Dar es salaam.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.