Polepole amjibu Nyalandu
Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amemponda aliyekuwa Mbunge wa
Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akisema walishamweka pembeni kwa kuwa hakuwa
mtu wa muhimu kwao.
Akizungumza
jana Jumatatu usiku katika kipindi cha Msemakweli kinachorushwa na Channel Ten,
Polepole aliyekuwa akizungumzia mafanikio ya Rais John Magufuli kwa kipindi cha
miaka miwili, alimtakia heri Nyalandu huku pia akisema amejimaliza mwenyewe.
“Ameondoka
mwanachama mmoja wa CCM leo (jana) amekwenda upinzani. Katiba yetu hii ya
Jamhuri ya Muungano inasema kila mtu ana uhuru wa kujiunga na chama chochote.
Tunaheshimu uamuzi wake, tunamkatia heri katika chama anakokwenda,” alisema
Polepole.
“Aliyeondoka
leo ni ‘very insignificant’ yaani kwa Kiswahili hatujaona utofauti. Ndiyo maana
sisi tumetoa maelekezo kwa Serikali kwamba, watu ambao hawakuweza kutukimbiza
katika awamu ya tano kwenye maendeleo ya Taifa letu kwenye uongozi wa awamu ya
tano wawekwe benchi kwanza. Sasa wamewekwa benchi,” alisema Polepole.
Hata hivyo
alisema Nyalandu ana haki ya kikatiba kuamua kwenda chama chochote anachokitaka
na kwa kuwa CCM ni chama cha kidemokrasia hakitamlazimisha kubaki.
Comments
Post a Comment