KESI YA KULIWA KWA KANUMBA KUANZA TENA
Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya kesi za mauaji ya bila kukusudia iliyotolewa na Mahakama Kuu, kesi ya Lulu itaanza kusikilizwa siku ya Oktoba 19/2017 mbele ya Jaji Sam Rumanyika.
Lulu anakabiliwa na kesi hiyo akidaiwa kumuua Msanii mwenzake, Steven Kanumba bila kukusudia kinyume cha kifungu cha 195 cha kanuni za adhabu (PC), April 7/2012 nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican.
Lulu na Kanumba walidaiwa kuwa ni wapenzi ambao mapenzi yao yalikuwa na siri kubwa mpaka tukio la kifo lilipomkuta Kanumba ndipo ilipofahamika juu ya mahusiano yao.
Comments
Post a Comment