Wakazi wa mtaa wa Kalamata katika kata ya Chemchem Halamshauri ya Manispaa ya Tabora wamelalamikia kuwepo kwa dimbwi lililojaa maji hali ambayo inahatarisha usalama wa wakazi hao hasa watoto
Na Mussa Mbeho,Tabora.
Wakazi wa mtaa wa Kalamata katika kata ya Chemchem Halamshauri ya Manispaa ya Tabora wamelalamikia kuwepo kwa dimbwi lililojaa maji hali ambayo inahatarisha usalama wa wakazi hao hasa watoto
Malalamiko hayo yametolewa na baadhi ya wakazi wa mtaa huo wakati wakizungumza na Mpanda fm mapema hii leo
Wamesema Dimbwi hilo limekuwa ni kero kubwa kwao ambapo mpaka sasa watu watano wametumbukia na kuumia vibaya.
Aidha Mpanda fm imemtafuta mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa kalama Mufti Hamidu Rashidi na kuzungumza nae juu ya mipango ya kulifukia Dimbwi hilo ambapo amesema wako katika mipamgo ya kurekebisha eneo hilo .
Kwa upande wake Diwani wa kata ya chemchem Bi Rehema Kabata amesema mbali na kulifukia dimbwi hilo wanatarajia kuweka daraja katika eneo hilo ili kuondoa kero hiyo kwa wakazi hao .
Kwa mujibu wa Diwani huyo barabara ya sabasaba uliopo mtaa wa Kalamata ni miongoni mwa barabara zinazokarabatiwa kupitia kwa ufadhili wa fedha kutoka mfuko wa benki ya dunia hivyo changamoto hiyo itamalizika baada ya ujenzi huo kukamilika .
Comments
Post a Comment