CCM SINGIDA YAMJIBU NYALANDU
Singida.
Chama cha Mapinduzi (CCM)
Mkoa wa Singida kimesema sababu zilizotolewa na aliyekuwa Mbunge wa Singida
Kaskazini, Lazaro Nyalandu za kuacha ubunge hazina mashiko, isipokuwa
kilichomsukuma kufukia uamuzi huo ni hasira za kukosa uwaziri.
Katibu wa CCM mkoani Singida, Jamson
Mhagama alisema jana Jumatatu Oktoba 30,2017 kuwa, “Kwa maono yake ameona siasa
za nchi haziendi vizuri na kuamua kwenda kusaka siasa zitakazompendeza,
tunamtakia kila la kheri. Ila tunamwonya kuwa asitarajie tena kupata ubunge kupitia
Chadema anakolilia kwenda, CCM itashinda kwa kishindo katika uchaguzi mdogo
ujao,” alisema.
“Wananchi walimwamini Nyalandu katika
vipindi vyote vinne kwa kumpa kura za kutosha za nafasi ya ubunge. Kupitia kura
hizo, Nyalandu amesifika na kujulikana kila kona sasa ameamua kuwapa kisogo
wakazi wa jimbo la Singida Kaskazini, jina lake linaenda kufutika na hatasikika
tena,” amesema Mhagama.
Comments
Post a Comment