Watanzania wawili kunyongwa China, mtoto arudishwa
Watanzania wawili mume na mke waliotambulika kwa majina ya Baraka Malali na mkewe Ashura Mussa wamekamatwa na dawa za kulevya China katika uwanja wa ndege wa Baiyun Guangzhou wakiwa na mtoto wao mdogo wa miaka 2 ambaye amerudishwa leo nchini Tanzania Taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Sheria za Madawa ya kulevya, Edwin Kakolaki amesema kuwa raia hao wa Tanzania Januari 19, 2018 uwanja wa ndege wa Baiyun Guangzhou, wakiwa wamemeza tumboni dawa za kulevya, walihifadhiwa kwenye chumba maalum kwa muda, Baraka alitoa pipi 47 kwa njia ya haja ambapo mkewe alitoa pipi 82. Serikali ya China iliwasiliana na serikali ya Tanzania kuhusiana na suala la mtoto huyo ambapo walikubaliana kumrudisha mtoto huyo nchini, mtoto huyo amewasili leo nchini Tanzania na Serikali kusema kuwa watafanya utaratibu wa kuhakikisha wanawatafuta ndugu wa watu hao ili waweze kuwakabidhi mtoto huyo. Aidha Kakolaki amewataka Watanzania kuendelea kuwaombea wazazi ha...