Wananchi mkoani Katavi wawalaumu viongozi kushindwa kutatua tatizo la ukosefu wa maji safi na salama



NSIMBO

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kapanda halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wameutuhumu uongozi wa kijiji hicho kwa kushindwa kushughulikia utatuzi wa tatizo la  uhaba wa maji safi na salama.

Kwa kiasi kikubwa wahanga wa tatizo hilo wakiwa ni wanawake wameiambia Mpanda radio, kuwa muda mwingi unatumika kutafuta maji kuliko kufanya shughuli za kimaendeleo.

Mmoja wa viongozi Bw Maiko Chananza amekiri kuwepo kwa tatizo hilo huku akizitupia lawama mamlaka zingine kwa kushindwa kuwajibika.

Sera ya maji ya taifa inataka maeneo ya vijijini maji yapatikane kila umbali wa mita 400 jambo ambalo mpaka sasa limebaki na utata.


Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI