Baadhi ya wanawake mkoani katavi wamesema wanashindwa kutumia njia za uzazi wa mpango kutokana na kukosa elimu sahihi juu ya uzazi.






MPANDA

Baadhi ya wanawake mkoani katavi wamesema wanashindwa kutumia njia za uzazi wa mpango kutokana na kukosa elimu sahihi juu ya uzazi.

Wanawake hao wameiambia mpanda Radio kuwa  moja ya changamoto ni imani potofu na baadhi ya wanaume kutotaka kushiriki katika njia za uzazi wa mpango.

Kwa upande wake muuguzi anayesimamia huduma ya baba,mama na mtoto katika zahanati ya kata ya Kakese Yusuph Jabil Ally amesema kuwa wanawake wengi wamekuwa wanaogopa kupata ushauri juu ya ya njia salama za uzazi wa mpango

Bwana Ally ametoa wito kwa wakazi kuachana na imani potofu juu njia za uzazi wa mpango ili kujikinga na mimba zisizotarajiwa na kupanga familia ya watoto ambao watakuwa na uwezo wa kuwatunza.


Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI