Rais Magufuli awatunuku kamisheni maofisa197 wa Jeshi la wananchi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatunuku kamisheni maofisa wanafunzi 197 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Sherehe hizo zimefanyika leo Februari 3, 2018 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam, ambapo maofisa hao wapya ni wa Tanzania na kutoka nchi marafiki, waliopata mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli mkoani Arusha.
Katia tukio hilo ambalo lilipambwa na magwaride kutoka kwa Wanajeshi hao, lilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Kitaifa.
Miongoni mwa waliotunukiwa kamisheni hizo wanawake ni 28, na waliobaki ni wanaume.
Comments
Post a Comment