Halmashauri ya manispaa ya Mpanda imenunua lori jipya la kuzoa taka ili kukabiliana na mrundikano wa takataka mji hapa.



MPANDA

Halmashauri ya manispaa ya Mpanda imenunua lori jipya la kuzoa taka ili kukabiliana na mrundikano wa takataka mji hapa.

Akizungumza wakati wa kukabidhi lori hilo kwa meya wa manispaa ya mpanda William Mbogo mkuu wa wilaya ya Mpanda bi lilian matinga amepongeza hatua hiyo na kuiomba manispaa kulitunza gari hilo

Kwa upande wake Mstahiki meya wa manispaa ya Mpanda William Mbogo ameto shukrani kwa baraza la madiwani kwa kukubali wazo la kubadili fedha za ununuzi wa lori hilo ambazo awali zilielekezwa kununua gari la Meya wa Manispaa

Kwa mjibu wa Kaimu mkuruingenzi wa Manispaa ya Mpanda Deodatus Kangu, amesema fedha zote sh milioni 159 zilizotumika kununua gari hilo ni makusanyo ya ndani ya manispaa na kueleza jinsi lori hilo litakavyosaidia katika uzoaji wa taka

Manispaa ya Mpanda huzalisha kiasi cha taka tani sabini nukta tano kwa siku hivyo kununuliwa kwa lori hilo lenye uwezo wa kubeba tani 16 linatarajiwa kuondoa mrundikano wa taka katika vizimba mbalimbali

 

 


Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.