Polisi watakao Pokea Rushwa kukiona cha moto



KATAVI

Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Katavi RTO John Mfinanga amesema hatamfumbia macho asikali yeyote wa Usalama barabarani atakaye jihusisha na kupokea rushwa ikiwemo uvunjaji wa sheria wakati wa majukumu.

Hayo yanajili leo ikiwa kesho utafanyika uzinduzi wa Wiki ya nenda kwa Usalama mkoa wa Katavi ambapo ameeleza kuwa elimu ya Usalama barabarani itajumuisha wadau mbali mbali, kama vile Madereva piki piki,  chuo cha ufundi Veta, Wakala na wananchi.

Katika hatua nyingine amewataka waendesha vyombo vya moto kujitokeza ili waendelee kupata elimu ikiwemo mikakati ya Jeshi hilo katika kuimarisha hali ya Usalama barabarani.

Kwa upande wa mwenyekiti wa Chama cha boda boda mkoa wa Katavi Stefano Asalile Mwakabafu amewataka waendesha piki piki wote kuwa na kofia mbili ngumu Helmet kwaajili ya dereva na abiria.

Kauli Mbiu ya Wiki ya Nenda kwa usalama ni Tii  Sheria Ukoa Maisha Kataa Rushwa.

Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI