Chama cha walemavu mkoa wa katavi manispaa ya Mpanda (SHIZAWATA) kimesema kuwa mpaka sasa hakijapatiwa pesa za mkopo kwa walemavu kutoka Manispaa.


MPANDA

Chama  cha walemavu mkoa wa katavi manispaa ya Mpanda (SHIZAWATA)  kimesema kuwa mpaka sasa  hakijapatiwa pesa za mkopo kwa walemavu kutoka Manispaa.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa walemavu shirikisho la wasioona mkoa wa katavi bwana Izack Lukasi Mlela wakati akizuingumza na mpanda radio ofisini kwake.

Hata hivyo bwana Izack amesema kuwa serika;li imewapatia maeneo yakufanyia biashara za ujasiriamali katika soko la misunkumilo lakini  mpaka sasa haijawakabidhiwa kutokana na vikundi vya walemavu ambavyo vilikuwa vimesajiliwa  kutowezeshwa.

Halmashauiri ya manispaa ya Mpanda ilitangaza kutenga kiasi cha asilimia 2 kutokana na mapato yake ya ndani kwa ajili ya kuwawezesha watu wenye ulemavu  kila mwaka.


Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.