Mwanasheria mkuu wa Kenya Profesa Githu Muigai amejiuzulu baada ya kuhudumu kwa miaka sita na nusu.
NAIROBI
Mwanasheria
mkuu wa Kenya Profesa Githu Muigai amejiuzulu baada ya kuhudumu kwa miaka sita
na nusu.
Rais Uhuru Kenyatta amemshukuru Profesa Githu kwa
huduma zake na sasa jaji Paul Kihara Kariuki atachukua mahala pake.
Rais Uhuru Kenyatta amemshukuru kwa huduma yake
katika kipindi cha miaka sita na nusualichotumika kama mwanasheria mkuu .
Ujumbe ambao umeandikwa katika mtandao wa twitter
na jaji Paul Kiharara umeeleza hayo.
Wakati wa vugu vugu la upinzani kushinikiza
mwanasiasa kinara wa muungano wa NASSA
Raila Odinga kujiapisha kama rais wa wananchi wa Kenya Profesa Githu Muigai
alikosoa jambo hilo na kuliita uhaini ambao adhabu yake ni kifo.
Comments
Post a Comment