Makamu wa Rais, Mh. Mama Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali inajitahidi kujenga na kutanua vituo vya Afya ili kupunguza msongamano kwenye hospitali za Wilaya.
Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo leo wakati wa kuweka jiwe la msingi la upanuzi wa kituo cha Afya Ihongole kilichopo mjini Mafinga.
Mh. Samia ambaye yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Iringa leo ametembelea Wilaya ya Mufindi na kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili ikiwa mmoja ni wa kujenga maabara ya kisasa na madarasa ya kidato cha tano na sita katika Sekondari ya Mgololo na upanuzi wa kituo cha Afya cha Ihongole kilichopo Mafinga.
Akiwahutubia wananchi, amesema katika kila kituo cha afya kinachopanuliwa ama kujengwa, Serikali imezingatia huduma za mama na mtoto ili kupunguza vifo vya akinamama na watoto, na kuborsha huduma za upasuaji .
Serikali imetoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho na kutumia mafundi wa kawaida kujenga ili kuweza kusaidia kutoa ajira kwa vijana zaidi wa eneo husika.
Comments
Post a Comment