CHADEMA wadai kunyimwa uwanja kumuaga Tambwe
Mashinji amesema hayo leo Februari 10, 2018 wakati wa kuaga mwili wa Richard Tambwe tukio ambalo limefanyika nyumbani kwa marehemu Mbagala jijini Dar es Salaam na baadae kwenda kupumzishwa mwili wake katika makaburi ya Chang'ombe.
"Ndugu waombolezaji Taifa letu linaanza kujifunza ustaraabu mpya ambao sisi tuliopo hapa tunatakiwa tuchague kuupenda au kuuchukia kwa sababu uchaguzi huu utabaki kuwa kwetu lakini siyo kwa wale wanaotufundisha ustarabu huu, tumetumia siku mbili tunazunguka kutafuta viwanja ila kila sehemu ukigusa wanasema CHADEMA siasa, baadae mpaka kikao cha jana jioni tumekaa hapa na kaka zangu hapa tukasema lakini huyu si alikuwa na nyumbani kwake? Sasa hata hapa nyumbani watatuambia ni siasa? Sasa huu ni ustarabu mpya tunaanza kufundishwa katika Taifa letu, ustarabu wa kuanza kuogopana, ustarabu wa kuanza kupeana makundi kwamba huyu ni wao sisi ni sisi" alisema Mashinji
Mbali na hilo Mashinji alidai kuwa wiki tatu zilizopita alimwita Tambwe ofisi kwake baada ya kushauriwa kuwa angemtumia katika kutengeneza mpango wa Uenezi ndani ya Chama chao na kudai kuwa kiongozi huyo alimuahidi kuwa ataifanya kazi hiyo baada ya uchaguzi wa marudio katika jimbo la Kinondoni ambao unatarajiwa kufanyika Februari 17 mwaka huu lakini kwa bahati mbaya umauti umemfika kabla ya uchaguzi huo.
Comments
Post a Comment