Posts

Showing posts from January, 2018

Rais Wa Tanzania DK John Pombe Magufuli azindua hati ya kusafiria ya Kielektroniki

Image
DAR ES SALAAM: Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli   amesema   uzinduzi wa hati ya kusafiria ya kierektroniki utamaliza changamoto za usafiri nnje ya nchi ikiwemo biashara haramu za madawa ya kulevya. Uzinduzi huo umehudhuriwa na wageni wengine ambao ni Makamu wa rais wa Tanzania   Mama Samiah Suluh, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk Mohamed Shein na viongozi wengine wa Serikali. Aidha ameelezea kuwa uwajibikaji wa serikali awamu ya tano ni chachu ya maendeleo hayo yaliyofikiwa katika kuimarisha uchumi wa Tanzania kwa kuangazia utatuzi wa vikwazo vya kibiashara nnje ya Tanzania. Katika hatua nyingine ameitaka idara ya Uhamiaji kujitathimini katika utendaji wake akitolea mfano wa ukamatwaji wa mamia ya wahamiaji haramu nchini katika mikoa ya Mbeya na Iringa . Hati ya kusafiria ya kierektoniki itapatikana kwa kiasi cha shiringi laki moja na nusu.

Umeme wa Jenereta Katavi mwisho mwaka 2020

Image
KATAVI Miaka miwili ijayo shirika la umeme tanesko mkoa wa Katavi litaachana na uzalishaji wa nishati ya   umeme kwa Jenereta na kujiunga na griidi ya Taifa. Waziri wa nishati Dr Merdard Kareman   ameeleza hayo wakati akikagua mradi wa mashine za kuzalisha umeme katika kata ya Inyonga   wilaya ya Mlele   mkoani katavi huku akishukuru kazi nzuri inayofanywa na Tanesco. Katika hatua nyingine amesema miezi kufikia mwaka 2019 vijiji vingi mkoani Katavi vitafikiwa na umeme ili kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia msukumo wa vyawanda ambavyo hutegea uwepo wa nishati ya umeme. Mkoa wa Katavi unawilaya Tatu ambazo ni Wilaya ya Mpanda, Tanginyika na Mlele lakini Mpaka sasa shirika la Tanesko hutumia Jenereta kama chanzo cha nishati ya Umeme. PAUL MATIUS

Odinga aongeza Idadai ya Viongozi walio wahi jiapisha wenyewe

Image
NAIROBI: Raila Odinga mwanasiasa wa upinzani wa Kenya anaongeza orodha ya Viongozi   waliowahi ku ji a p isha na kujitangaza kuwa marais kama huku kukiwa na rais Mamlakani. Raila Odinga amejiapisha kuwa 'rais wa wananchi' nchini humo baada ya kusema hatambui ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa marudio uliofanyika nchini humo Oktoba mwaka jana. Mgombea mwenza   Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper hakujitokeza katika sherehe hiyo ya kiapo ingawa alikuwa miongoni mwa waliotarajiwa kuapishwa. Waziri mkuu huyo wa zamani ni miongoni mwa viongozi wa kisiasa walio jaribu kujitangaza marais,   huku kukiwa bado kuna rais mwingine madarakani. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Etienne Tshisekedi, Nigeria Moshod Abiola, Uganda Kiza Besigye na Jean Ping wa Gabon ni miongoni mwa viongozi wa upinzani wa Afrika ambao wamejaribu kujitangaza kuwa marais, na sasa Raila Odinga amejiunga na orodha hii. Source BBC

Walimu walio kaidi agizo la Rais Magufuli wasimamishwa kazi

Image
Halmshauri ya wilaya ya Magu mkoani Mwanza imewasimamisha kazi walimu watatu wa shule ya msingi Nenge akiwemo Mwalimu Mkuu na Afisa Elimu Kata ya Nyanguge kwa kosa la kukaidi agizo la Rais Magufuli la kutochangisha fedha wanafunzi. Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Magu Lutengano Mwalwiba, amesema kuwa baada ya agizo la Rais Magufuli la kusitisha michango katika shule za msingi, Januari 23 mwaka huu aliwaonya wakuu wa shule na walimu wote, lakini Januari 24 waliendeleza kukusanya michango. Mwalwiba meongeza kuwa watumishi hao wamekiuka mkataba wa elimu ya msingi bila malipo ambapo wamewachangisha shilingi 500 wanafunzi 378 wa shule hiyo kwa ajili ya lebo zautambulisho wa sare za wanafunzi kinyume na maagizo ya Rais Magufuli.  January 17 mwaka huu Rais John Pombe Magufuli alipiga marufuku michango kwenye shule za msingi na sekondari za serikali, na kuwaagiza Mawaziri Joyce Ndalichako na Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jafo kusimami...

Raila Odinga amejiapisha kuwa rais wa wananchi .

Image
Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA Raila Odinga, amejiapisha kuwa rais wa Jamhuri ya watu wa Kenya mbele ya wafuasi wake katika bustani ya Uhuru jijini Nairobi. Odinga amechukua hatua hii licha ya onyo la serikali ya rais Uhuru Kenyatta kuwa itamfungulia mashtaka ya uhaini. “Mimi Raila Amollo Odinga, nikiwa natambua wito, naapa kuwa rais wa Jamhuri ya watu wa Kenya,” alisema Odinga huku akishangiliwa na wafuasi wake. Kiongozi huyo aliwasili katika bustani hiyo bila ya naibu wake Kalonzo Musyoka ambaye awali aliripoti kuwa serikali ilikuwa imempokonya walinzi wake. “Kalonzo, Mudavadi na Wetangula hawapo hapa, lakini wako pamoja nasi, mtafahamishwa ni kwanini hawakufika,” alisema Odinga Akiwahotubia wafuasi wake, Odinga amesema wananchi wa taifa hilo wameamua kuondoa utawala wa kidikteta ulioletwa na wizi wa kura. Aidha, amesema kuwa ametimiza ahadi aliyoitoa kwa Wakenya kuwa ataapishwa kama rais wa wananchi.

Katika kuendana na mabadiliko ya teknolojia nchini mahakamaimeanzisha mfumo wa matumizi ya teknolojia habari na mawasiliano tehama ili kuewza kuendana na wakati pamoja na kutoa huduma kwa wanachi kwa haraka

Image
MWANZA Katika kuendana na mabadiliko ya teknolojia nchini mahakamaimeanzisha mfumo wa matumizi ya teknolojia habari na mawasiliano tehama ili kuewza kuendana na wakati pamoja na kutoa huduma kwa wanachi kwa haraka Haya yamejiri wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria ambapo mkuu wa mkoa wa mwanza John Mongela ameipongeza mahakama kwa hatua yao ya kwenda na wakati kwa kutumia mfumo huo wa tehama Amesema tehama inakwenda kuwa suruhisho katika kutoa huduma kwa haraka huku akileza wiki hii ya sheria itakuwa na mafanikio makubwa kwa wananchini na mkoa wa mwanza pamoja na taifa kwa ujumla Wiki ya sheria mwaka huu ina kauli mbiu imesemayo matumizi ya tehama katika utoaji wa haki kwa wakati na kwakuzingatia madili na kilele chake itakuwa tarehe moja mwezi wa pili mwaka  huu wa 2018 SOURCE Salum yasini

Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Muhuga aagiza viwanda 20 kila halmashauri

Image
KATAVI: Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga ameagiza Halamshauri zote tano za mkoa wa Katavi kuhakikisha kila moja inaanzisha viwanda 20 katika kipindi cha mwaka mmoja. Akizungumza katika kipindi cha kumekucha Tanzania cha Mpanda radio,amesema ifikapo Machi 30 mwaka huu  anatarajia kupokea ripoti ya mikakati ya halmashauri zote za mkoa ili kujua mipango iliyopangwa kwa ajili ya utekelezaaji. Aidha Muhuga amesema changamoto ya ukosefu wa umeme wa uhakika pamoja na miundombinu ya usafirishaji kama barabara na reli ni miongoni mwa changamoto ambazo bado ni kikwacho cha ukuaji wa uchumi wa haraka. Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amesema kuanzia mwezi ujao,kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa inatarajia kutembelea halamshauri zote za Mkoa ili kukagua hatua zilizofikiwa katika kuendesha mazao ya kilimo cha biashara yaliyoagizwa kulimwa kama mbadala wa zao la tumbaku.

Basi lawaka moto leo

Image
Basi la kampuni ya Tahmeed ambalo linafanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Mombasa Nairobi limeteketea moto katika kijiji cha Matumbi mkoani Tanga leo. Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Benedict Wakulyamba amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya moto na kusema kuwa hakuna abiria ambaye amepata madhara na moto huo ulioteketeza basi hilo. " Ni kweli basi hilo limewaka moto leo, ila hakuna abiria aliyejeruhiwa wala kupata madhara yoyote kwa kuwa dereva alipoona dalili za moto alipaki gari pembeni na abiri ambao walikuwepo kwenye basi hilo kama 15 hivi wote waliweza kushuka mapema kabla ya moto kushika gari zima"   alisema Wakulymba

NABII TITO APANDISHWA KIZIMBANI

Image
Tito Onesmo Machibya anayejulikana kama 'Nabii' Tito (44) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nong'ona Manispaa ya Dodoma leo Januari 29, 2018 amepandishwa mahakamani katika mahakama ya wilaya kwa shtaka la kutaka kujiua.  Nabii Tito amepandishwa kizimbani leo akidaiwa kutaka kujiua mwishoni mwa wiki jana ambapo alijichana chana na wembe katika baadhi ya maeneo ya mwili wake wakati Jeshi la Polisi likifanya uchunguzi nyumbani kwake.  Januari 23, 2018 Nabii Titoo alikamatwa na jeshi la polisi akituhumiwa kufanya uchochezi na baadaye alipelekwa kupimwa akili katika hospitali ya wagonjwa wa akili (Mirembe) na kufahamika kuwa mtu huyo alikuwa na matatizo ya akili, hivyo jeshi la polisi liliendelea kumshikilia kwa ajili ya usalama wake na siku jeshi hilo lilipokwenda kufanya uchunguzi nyumbani kwake ndipo alifanya jaribio la kutaka kujiua. 

'Kwa hili CHADEMA mnajisumbua''

Image
Mbunge wa Iramba Magharibi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema atawashangaa sana kuona wananchi wa jimbo la Kinondoni wakimpigia kura mgombea wa CHADEMA Salum Mwalimu kwa madai Ilani inayofanya Mhe. Mwigulu ameeleza hayo leo wakati wa akizindua kampeni hizo za uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kinondoni ambapo upande wa CCM wamemsimamisha mgombea Mtulia Said Maulid ambaye hapo awali yeye ndiye alikuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia CUF kabla hajajivua unachama wake na kuenda kumuunga mkono Rais Magufuli katika kujenga Taifa la Tanzania. "Msije mkaenda kupiga kura ya uchaguzi mdogo kwa kiwango cha uchaguzi mdogo, twendeni tukapige kura kwa uzito ule ule kwamba ni jambo la msingi, la kitaifa na jambo la chama chetu lenye maslahi mapana nalo. Tutakapo tawanyika hapa kila mmoja awe kampeni meneja wa mgombea wetu na aje na wapiga kura siku hiyo ya kupiga kura",  alisema Mwigulu. Pamoja na hayo, Mwigulu amedai CCM inasababu zot...

LOWASAAMCHANA MTULIA

Image
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa amewataka  wanachama na viongozi wa CHADEMA kuacha kumtaja taja mgombea Ubunge wa CCM Kinondoni Maulid Mtulia kwani mtu huyo ni wa hovyo hastaili kutajwa tajwa kwani kufanya hivyo ni kumpa kichwa.  Lowassa amesema hayo leo Januari 27, 2018 akiwa katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa marudio katika jimbo la Kinondoni ambapo leo maelfu ya wananchi wa Kinondoni wameweza kuwasikiliza viongozi mbalimbali wa CHADEMA kwa hoja na sera mbalimbali kuelekea uchaguzi huo ambao unatarajiwa kufanyika Februari 17, 2018.  "Kwanza nawashauri huyu Mtulia msimseme seme sana wanini huyu, mtu hovyo kabisa huyu mnampa kichwa tu sasa mtu hovyo hapaswi kuchukua muda wenu kumjadili bali nachotaka tushughulike kuwaelimisha wananchi wa Kinondoni kwanini wanastahili kutupa sisi kura, habari ya huyu bwana tuachane naye, hawa CCM hawaeleweki kule Moshi na Korogwe tulishinda lakini wakaja kusema tumeshindwa hivyo nataka ...

Mkuu wa zamani wa TBC Tido Mhando afikishwa mahakamani Dar es Salaam

Image
\Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC, Tido Mhando amefikishwa mahakamani leo jijini Dar es Salaam kwa mashtaka ya matumizi mabaya ya Madaraka. Tido Mhando, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Azam Media alifikishwa katika mahakama ya Kisutu mapema leo Ijumaa, na kusomewa dhidi mashtaka yake. Wakili wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) Leonard Swai aliambia hakimu mkazi mkuu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Victoria Nongwa kuwa Mhando anatuhumiwa kwa mashtaka matano. Anadaiwa kutenda makosa hayo mwaka 2008 alipokuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC. Anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka, wakati alipokuwa akilitumikia shirika hilo la Utangazaji la Serikali TBC, pamoja na kulitia hasara ya shilingi 897 milioni za Tanzani Kesi imeahirishwa hadi Februari 23, 2018 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali. Sheria nchini Tanzania haiwaruhusu washtakiwa, mawakili au watu wengine kuzungumzia kesi nje ya mahakama. Mhando ni miongoni mwa waandishi wa...

Zaidi ya asilimia 90 za watanzania wanatumia nishati ya mkaa kupikia hali inayopelekea kupunguza miti ya asili nchini hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira.

Image
DODOMA: Zaidi ya asilimia 90 za watanzania wanatumia nishati ya mkaa kupikia hali inayopelekea kupunguza miti ya asili nchini hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira. Hayo yamezungumzwa na waziri wa nchi ofisi ya makamu wa raisi mazingira na muungano mheshimiwa January Makamba wakati wa kampeni ya   upandaji miti mkoani Dodoma ameeleza kuwa asilimia 61 nchini ipo hatarini kuwa sehemu ya jangwa kutokana na ukataji wa miti ya asili. Waziri Makamba amesema kuwa ofisi ya makamu wa raisi imeaandaa mpango wa kutoa muda kwa taasisi kubwa za serikali ikiwemo magereza,shule na JKT kupewa muda kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja kuhama kutoka katika matumizi ya mkaa na badala yake kutumia gesi. Sheria ya mazingira ya Tanzania katika kifungu cha 13 ca sheria ya mazingira   inampa mamlaka waziri mwenye dhamana ya mazingira kutoa maelekezo kwa taasisi yeyote ya binafsi au ya umma kufanya jambo litakalo okoa mazingira.

Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi yatoa Onyo kali kwa Watendaji

Image
MPANDA:   Baraza la Madiwani Halamshauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,limesema litachukua hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafukuza kazi watumishi wa idara ya ardhi watakaosababisha migogoro ya ardhi baina ya wananchi. Tamko hilo ambalo limetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Willium Mbogo kupitia kikao maalumu cha bajeti cha baraza hilo ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo. Aidha amesema hatua za kisheria zitachukuliwa pia kwa watumishi wa idara mbalimbali ambao wamesababisha Manispaa ya Mpanda Kukosa mapato kutokana na uzembe wao katika uwajibikaji.    

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Michael Nzyungu,amekanusha taarifa zilizotangazwa na kituo cha Televisheni cha Azam ambacho kuwa Halmashauri haijafikia malengo ya makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Image
MPANDA Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Michael Nzyungu,amekanusha taarifa zilizotangazwa na kituo cha Televisheni cha Azam ambacho  kuwa Halmashauri haijafikia malengo ya makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2017/2018. Bw.Nzyungu ametoa ufafanuzi huo wakati akizungumza na Vyombo vya habari Ofisini kwake. Aidha Bw.Nzyungu pamoja na mambo mengine amevishauri vyombo vya habari kutumia waandishi wenye umahiri wa kuandika habari ili kufikisha taarifa sahihi kwa jamii. Kwa mjibu wa MkurugenziTaarifa hizo zilichukuliwa kupitia kikao cha baraza maalumu la madiwani lililokuwa likijadili rasmu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019.

Zaidi ya 30 wafa katika ajali ya moto Korea Kusini

Image
Zaidi ya watu 30 wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya moto uliyotokea katika Hospitali moja nchini Korea Kusini. Hata hivyo maofisa wanasema idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka kutoka katika ya majeruhi hao. Imefahamika kuwa moto huo ulianzia katika chumba cha dharura cha Hospitali ya Sejong, kusini mashariki mwa nchi hiyo. Zaidi ya majeruhi 100 wanasemakana wamo katika jengo la hospitali hiyo Picha za mitandao ya jamii, zinaonyesha vikosi vya zima moto wakijaribu kukabiliana na moto huo huku kukiwa na moshi mkubwa. Mwaka jana watu 29 walikufa katika mji wa Echeon, Korea Kusini, na wengine kujeruhiwa baada ya moto kuzuka katika sehemu ya mazoezi ya wazi.

Trump apewa onyo

Image
Tajiri Bill Gates amemuonya rais wa Marekani Donald Trump kwa kauli mbiu yake ya "Marekani Kwanza" kuwa inaweza kuharibu uhusiano wake na Afrika. Bill Gates ametoa kauli hiyo katika mkutano wa dunia wa uchumi World Economic Forum  unaofanyika huko Davos nchini Switzerland ambapo amesema kunatakiwa kuwepo kwa uwiano wa wenye nguvu kubwa na nguvu kidogo na kuanisha kwamba asingependa kuona uwiano huo unapotea. Bill Gates amesema kwamba Marekani inaweza kupoteza ushawishi wake barani Afrika kwa nchi kama China ambazo zinazidi kuwekeza barani Afrika, Bill Gates ambaye anamfuko wake unaoitwa Bill & Melinda Gates Foundation, umekijihusisha kwa kiasi kikubwa kutoa huduma za afya katika nchi kadhaa barani Afrika. Lakini rais Trump amesema kwamba atakata msaada wa bajeti wa afya kwa takribani dola bilioni 2.2 katika mfuko wa dunia. Pia Trump aliwakasirisha viongozi wa Afrika bada ya kuyaita mataifa ya Afrika machafu kupindukia.

Mwalimu amchinja mtoto

Image
Mwalimu mmoja wa sekondari nchini Kenya Stephen Wachira Wangara mwenye umri wa miaka 43, amefikishwa mahakamani kwa kosa la kumuua mtoto wake wa miezi 7 kwa kumchinja kwa panga. Wakielezea mbele ya mahakama mashahidi watano wa tukio hilo wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya usalama Kaunti ya Kirinyaga, Maina Muriuki walimweleza Jaji Lucy Gitari wa Mahakama Kuu ya Kerugoya, jinsi mtuhumiwa huyo alivyoua mtoto wake, Bwana Maina aliieleza mahakama kuwa mwili wa mtoto huyo ulikuwa umeeekwa ndani ya gunia ukiwa na damu, nje ya nyumba ya Bw Wangara, na kando ya mwili huo kuliwa na panga ambayo ilitumiwa kumuua mtoto huyo. Shahidi mwingine Joseph Muriithi alisema wakati wa tukio hilo alikuwa shambani kwa Bw. Wangara akifanya kibarua, na mtuhumiwa huyo kwenda akiwa na madoa ya damu, na muda mfupi baadaye alisikia kelele kutoka kwenye nyumba ya mwalimu huyo. Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Machi 1, 2018, ambapo itasikilizwa tena. B...

Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi aendelea kusota lumande

Image
Kesi inayomkabili Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyassa, Emmanuel Masonga imeharishwa hadi kesho ambapo upande wa walalamikiwa wataanza kutoa utetezi wao. Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Mbeya Michael Mteite, baada ya kutupilia mbali pingamizi lililowekwa siku ya jana (Jumanne) na kuweza kusikiliza ushahidi huo wa sauti kwa takribani dakika 39 uliyotolewa na shahidi namba tano wa kesi hiyo Afande Joramu Magova ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama katika Ofisi ya Upelelezi Mkoani humo.  Kutokana na hilo Wakili  Mkuu wa  Serikali Joseph Pande, ameieleza Mahakama kuwa wameamua kufunga ushahidi upande wa Jamhuri kwa kuwa hawaoni sababu ya kuendelea na mashahidi wengine mara baada ya kuridhika na shahidi namba tano wa Afande Joramu Magova, ambaye alikuwepo kwenye mkutano  na kurekodi sauti kwa kutumia kinasa sauti. Hata hivyo Wakili wa utet...

Kifo cha kikatili kwa mwanafunzi mkoani Katavi cha wa gadhabisha Wananchi

Image
TANGANYIKA: Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi V ikonge K ata ya tongwe   wilaya ya Tanganyika mkoani katavi mwenye umri wa miaka 14 amefariki dunia baada ya kubakwa kisha kubakwa. K amanda wa polisi mkoa wa K atavi Damas Nyanda  ameeleza kuwa tukio hilo limetokea tarehe 22 majira ya saa mbili asubuhi wakati msichana huyo akiwa na mdogo wake wa kiume kuelekea shuleni. Insert……Kamanda Ameongeza kusema upelelezi unaendelea ilikuwabaini walio husika na kitendo hicho cha ukatili ili mkondo wa sheria uchukue nafasi yake . Wananchi wamegadhabishwa na kitendo hicho wengi wakilitaka jeshi la polisi kuwatia nguvuni wahalifu hao mara moja. Katika hatua nyingine kamanda huyo amekemea vikali kwa wale wote wanaomiliki silaha kinyume n a sheria akiwataka kuzisalimisha jeshi la polisi.

Shambulio la kigaidi laua watu 27 Libya

Image
TRIPOL: Takriban watu 27 wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa karibu na msikiti mmoja katika mji wa Benghaz nchini Libya utokana na shambulio la kigaidi. Milipuko hiyo miwili nje ya msikitiki karibu na eneo la Al Suleiman imetokea katika swala ya maghari,ambapo waumini hao wakati wanatoka ndani ya msikiti ndipo walipolengwa na shambulio hilo. Vipande vya picha za video zilizoonyeshwa kupitia Televishen ya taifa,zimeonesha miili ya watu waliouawa katika shambulio hilo ikiwekwa ndani ya gari la Polisi. Katika shambulizi hilo gari la kwanza lilifika wakati waumini wakitoka na kulipuka,ambapo gari la pili katika shambulizi hilo lililipuka muda mfupi upande wa pili wa mtaa huo dakika chache baadaye lililo beba vilupuzi Wanajeshi pamoja na raia ni miongoni mwa watu waliathiriwa na shambulizi hilo.Hata hivyo idadi ya watu waliojeruhiwa na vifo huenda ikapanda kutokana na watu wengi kujeruhiwa. souece RFI

Chadema ya mshitaki mkuu wa wilaya

Image
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepanga leo kupeleka mashataka yake katika Kamati ya Maadili kumshataki Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu ambaye alishiriki kufanya kampeni kumnadi mgombea wa CCM jimbo la Siha.  Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amethibitisha hilo na kusema kuwa leo majira ya saa tano asubuhi watafikisha mashtaka yao kwenye Tume ya Maadili kama ambavyo wameshautiwa na Tume ya Uchaguzi (NEC). " Tunapeleka mashtaka leo kwenye kamati ya maadili, tulipanga kupeleka saa tano asubuhi kwa hiyo mashtaka yatakwenda muda huu kumshtaki rasmi Mkuu wa Wilaya"  alisema Mrema  Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu alipanda jukwaani kumnadi mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Siha, Dk Godwin Mollel, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu kwani Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa mikoa na Wakurugenzi hawapashi kushiriki katika masuala ya siasa, na hii imetokea ikiwa tayari Tume ya Uchaguzi i...

Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mkoani Katavi la kiri kushindwa kuitoa miili ya wachimbaji walio fukiwa na kifusi mgodini.

Image
Mwandishi wa habari Alinanuswe Edward akiwa katika eneo lililo karibu na shimo(Longbase) lilibomoka na kuwafukia wachimbaji wawili mmoja wapo akifahamika kwa jina la Azam Lawrence Nyembeke MPANDA: Miili ya vijana wawili waliofunikwa na kifusi cha udongo katika machimbo ya dhahabu yaliyo kijiji cha Ibindi  Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi bado haijaopolewa kwa wiki ya pili sasa. Mpanda radio imefika katika eneo la Kwa Songoro lililopo kijiji cha Ibindi na kuzungumza na baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo ambao wameelea kusikitishwa na tukio hilo. Kwa mujibu wa mashahidi wameiambia  Mpanda radio kuwa mmoja ya vijana waliopoteza maisha Azam Lawrence Nyembeke mkazi wa Iringa  ndugu zake hawana taarifa mpaka sasa. Viza ya dharura ambayo alikuwa a akiitumia marehemu Azam Lawrence Nyembeke Licha ya juhudi mbalimbali zilizofanywa na wachimbaji wakishirikiana na wananchi wa eneo hilo Jeshi la zimamoto na Uokoji mkoani katavi limekiri kushindwa kutoa miili hiyo kwa ...

Afariki akitoa sadaka kanisani

Image
RUKWA:  Mwanakwaya wa kwaya ya Mtakatifu Secilia, Kigango cha Muze Parokia ya Zimba, Jimbo Katoliki Sumbawanga, Flora Nandi (25) ameanguka na kufariki dunia muda mfupi baada ya kutoa sadaka ya shukrani akiwa kanisani. Tukio hilo limetokea siku ya  Jumapili  saa nne za asubuhi wakati wa ibada ya kwanza , kwaya ya Mtakatifu Secilia  ikimsifu Mungu katika ibada hiyo. Akizungumzia tukio hilo, mwalimu wa kanisa aliyekuwa akiongoza ibada hiyo, Katekista Philipo Lupadasi amesema wanakwaya wakiwa wanaimba na marehemu akiwa ametoka kutoa sadaka ya shukrani na kuendelea kuimba ghafla alianguka chini hali iliyozua mshtuko na kusababisha ibada kusimama kwa muda. Amesema baada ya kufikishwa katika zahanati hiyo alipokewa na wahudumu wa afya ambao baada ya kumfanyia uchunguzi walibaini kuwa alikuwa ameshafariki dunia. Source Mwananchi

Rais Museveni wa Uganda asema anamkubali sana Trump

Image
KAMPALA: Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema anampenda rais wa Marekani Donald Trump katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa bunge la Afrika Mashariki jijini Kampala. Pongezi hizo za museven kwa Trump zinakuja saa chache tuu baada ya balozi wa Uganda kwa Marekani Deborah Malac kumkosoa Trump. Maoni hayo ya rais Museveni ni tofauti sana na viongozi wengi wanaochukizwa na kauli za Trump. Mapema mwezi huu Trump alidaiwa kutoa kauli za kejeli juu ya nchi za Afrika wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya wahamiaji. Trump a meyakanusha madai hayo lakini seneta mmoja aliyehudhuria mkutano huo a me sema kuwa Trump alitamka maneno ya kejeli na matusi kwa nchi kama Haiti, elsalvador na nchi za Afrika. Source BBC

Wananchi waomba kupelekewa umeme Mpanda

Image
NA: NEEMA MANYAMA Kata ya Magamba wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi inakabiliwa na ukosefu wa huduma ya umeme hali inayosababisha huduma duni katika vijiji hivyo. Akizungumza na Mpanda Radio diwani wa Kata hiyo Mh.Philipo Kalyalya amesema suala la ukosefu wa umeme katika kata hiyo limekuwa na changamoto kubwa hali inayopelekea kukwamisha  huduma mbali mbali za kijamii Kwa upande wake Meneja uhusiano wa tanesco mkoani hapa Bwn.Amon Michael amewataka wakazi katika maeneo hayo kwenda katika ofisi za Tanesco  kujiandikisha kwa ajili yakufungiwa umeme kabla bei hazijabadilika. Kata ya Magamba ni miongoni mwa kata zilizopitiwa na mradi wa rea ya awamu ya tatu baadhi ya maeneo mpaka sasa kutajwa kukosa huduma ya umeme.