Mwalimu amchinja mtoto
Wakielezea mbele ya mahakama mashahidi watano wa tukio hilo wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya usalama Kaunti ya Kirinyaga, Maina Muriuki walimweleza Jaji Lucy Gitari wa Mahakama Kuu ya Kerugoya, jinsi mtuhumiwa huyo alivyoua mtoto wake,
Bwana Maina aliieleza mahakama kuwa mwili wa mtoto huyo ulikuwa umeeekwa ndani ya gunia ukiwa na damu, nje ya nyumba ya Bw Wangara, na kando ya mwili huo kuliwa na panga ambayo ilitumiwa kumuua mtoto huyo.
Shahidi mwingine Joseph Muriithi alisema wakati wa tukio hilo alikuwa shambani kwa Bw. Wangara akifanya kibarua, na mtuhumiwa huyo kwenda akiwa na madoa ya damu, na muda mfupi baadaye alisikia kelele kutoka kwenye nyumba ya mwalimu huyo.
Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Machi 1, 2018, ambapo itasikilizwa tena.
Bw Wangara ambaye ni mtuhumiwa ni baba wa watoto wawili na mwalimu katika shule ya upili (sekondari) ya Gituya
Comments
Post a Comment