Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Muhuga aagiza viwanda 20 kila halmashauri
KATAVI:
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga ameagiza Halamshauri
zote tano za mkoa wa Katavi kuhakikisha kila moja inaanzisha viwanda 20 katika
kipindi cha mwaka mmoja.
Akizungumza
katika kipindi cha kumekucha Tanzania cha Mpanda radio,amesema ifikapo Machi 30
mwaka huu anatarajia kupokea ripoti ya
mikakati ya halmashauri zote za mkoa ili kujua mipango iliyopangwa kwa ajili ya
utekelezaaji.
Aidha
Muhuga amesema changamoto ya ukosefu wa umeme wa uhakika pamoja na miundombinu
ya usafirishaji kama barabara na reli ni miongoni mwa changamoto ambazo bado ni
kikwacho cha ukuaji wa uchumi wa haraka.
Katika
hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amesema kuanzia mwezi ujao,kamati ya ulinzi na
usalama ya mkoa inatarajia kutembelea halamshauri zote za Mkoa ili kukagua
hatua zilizofikiwa katika kuendesha mazao ya kilimo cha biashara yaliyoagizwa
kulimwa kama mbadala wa zao la tumbaku.
Comments
Post a Comment