Odinga aongeza Idadai ya Viongozi walio wahi jiapisha wenyewe



NAIROBI:

Raila Odinga mwanasiasa wa upinzani wa Kenya anaongeza orodha ya Viongozi  waliowahi kujiapisha na kujitangaza kuwa marais kama huku kukiwa na rais Mamlakani.

Raila Odinga amejiapisha kuwa 'rais wa wananchi' nchini humo baada ya kusema hatambui ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa marudio uliofanyika nchini humo Oktoba mwaka jana.

Mgombea mwenza  Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper hakujitokeza katika sherehe hiyo ya kiapo ingawa alikuwa miongoni mwa waliotarajiwa kuapishwa.

Waziri mkuu huyo wa zamani ni miongoni mwa viongozi wa kisiasa walio jaribu kujitangaza marais,  huku kukiwa bado kuna rais mwingine madarakani.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Etienne Tshisekedi, Nigeria Moshod Abiola, Uganda Kiza Besigye na Jean Ping wa Gabon ni miongoni mwa viongozi wa upinzani wa Afrika ambao wamejaribu kujitangaza kuwa marais, na sasa Raila Odinga amejiunga na orodha hii.

Source BBC


Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI