Zaidi ya asilimia 90 za watanzania wanatumia nishati ya mkaa kupikia hali inayopelekea kupunguza miti ya asili nchini hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira.
DODOMA:
Zaidi ya asilimia 90 za
watanzania wanatumia nishati ya mkaa kupikia hali inayopelekea kupunguza miti
ya asili nchini hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira.
Hayo yamezungumzwa na
waziri wa nchi ofisi ya makamu wa raisi mazingira na muungano mheshimiwa January
Makamba wakati wa kampeni ya upandaji
miti mkoani Dodoma ameeleza kuwa asilimia 61 nchini ipo hatarini kuwa sehemu ya
jangwa kutokana na ukataji wa miti ya asili.
Waziri Makamba amesema kuwa
ofisi ya makamu wa raisi imeaandaa mpango wa kutoa muda kwa taasisi kubwa za
serikali ikiwemo magereza,shule na JKT kupewa muda kwa kipindi kisichozidi
mwaka mmoja kuhama kutoka katika matumizi ya mkaa na badala yake kutumia gesi.
Sheria ya mazingira ya
Tanzania katika kifungu cha 13 ca sheria ya mazingira inampa mamlaka waziri mwenye dhamana ya
mazingira kutoa maelekezo kwa taasisi yeyote ya binafsi au ya umma kufanya
jambo litakalo okoa mazingira.
Comments
Post a Comment