Afariki akitoa sadaka kanisani


RUKWA:

 Mwanakwaya wa kwaya ya Mtakatifu Secilia, Kigango cha Muze Parokia ya Zimba, Jimbo Katoliki Sumbawanga, Flora Nandi (25) ameanguka na kufariki dunia muda mfupi baada ya kutoa sadaka ya shukrani akiwa kanisani.

Tukio hilo limetokea siku ya  Jumapili  saa nne za asubuhi wakati wa ibada ya kwanza , kwaya ya Mtakatifu Secilia  ikimsifu Mungu katika ibada hiyo.

Akizungumzia tukio hilo, mwalimu wa kanisa aliyekuwa akiongoza ibada hiyo, Katekista Philipo Lupadasi amesema wanakwaya wakiwa wanaimba na marehemu akiwa ametoka kutoa sadaka ya shukrani na kuendelea kuimba ghafla alianguka chini hali iliyozua mshtuko na kusababisha ibada kusimama kwa muda.

Amesema baada ya kufikishwa katika zahanati hiyo alipokewa na wahudumu wa afya ambao baada ya kumfanyia uchunguzi walibaini kuwa alikuwa ameshafariki dunia.

Source Mwananchi

Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI