Shambulio la kigaidi laua watu 27 Libya
TRIPOL:
Takriban watu 27 wamekufa na
wengine kadhaa kujeruhiwa karibu na msikiti mmoja katika mji wa Benghaz nchini
Libya utokana na shambulio la kigaidi.
Milipuko hiyo miwili nje ya
msikitiki karibu na eneo la Al Suleiman imetokea katika swala ya maghari,ambapo
waumini hao wakati wanatoka ndani ya msikiti ndipo walipolengwa na shambulio
hilo.
Vipande vya picha za video
zilizoonyeshwa kupitia Televishen ya taifa,zimeonesha miili ya watu waliouawa
katika shambulio hilo ikiwekwa ndani ya gari la Polisi.
Katika shambulizi hilo gari la
kwanza lilifika wakati waumini wakitoka na kulipuka,ambapo gari la pili katika
shambulizi hilo lililipuka muda mfupi upande wa pili wa mtaa huo dakika chache
baadaye lililo beba vilupuzi
Wanajeshi pamoja na raia ni
miongoni mwa watu waliathiriwa na shambulizi hilo.Hata hivyo idadi ya watu
waliojeruhiwa na vifo huenda ikapanda kutokana na watu wengi kujeruhiwa.
souece RFI
Comments
Post a Comment