Wananchi waomba kupelekewa umeme Mpanda


NA: NEEMA MANYAMA

Kata ya Magamba wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi inakabiliwa na ukosefu wa huduma ya umeme hali inayosababisha huduma duni katika vijiji hivyo.

Akizungumza na Mpanda Radio diwani wa Kata hiyo Mh.Philipo Kalyalya amesema suala la ukosefu wa umeme katika kata hiyo limekuwa na changamoto kubwa hali inayopelekea kukwamisha  huduma mbali mbali za kijamii

Kwa upande wake Meneja uhusiano wa tanesco mkoani hapa Bwn.Amon Michael amewataka wakazi katika maeneo hayo kwenda katika ofisi za Tanesco  kujiandikisha kwa ajili yakufungiwa umeme kabla bei hazijabadilika.

Kata ya Magamba ni miongoni mwa kata zilizopitiwa na mradi wa rea ya awamu ya tatu baadhi ya maeneo mpaka sasa kutajwa kukosa huduma ya umeme.

Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI