Umeme wa Jenereta Katavi mwisho mwaka 2020




KATAVI

Miaka miwili ijayo shirika la umeme tanesko mkoa wa Katavi litaachana na uzalishaji wa nishati ya  umeme kwa Jenereta na kujiunga na griidi ya Taifa.

Waziri wa nishati Dr Merdard Kareman  ameeleza hayo wakati akikagua mradi wa mashine za kuzalisha umeme katika kata ya Inyonga  wilaya ya Mlele  mkoani katavi huku akishukuru kazi nzuri inayofanywa na Tanesco.

Katika hatua nyingine amesema miezi kufikia mwaka 2019 vijiji vingi mkoani Katavi vitafikiwa na umeme ili kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia msukumo wa vyawanda ambavyo hutegea uwepo wa nishati ya umeme.


Mkoa wa Katavi unawilaya Tatu ambazo ni Wilaya ya Mpanda, Tanginyika na Mlele lakini Mpaka sasa shirika la Tanesko hutumia Jenereta kama chanzo cha nishati ya Umeme.

PAUL MATIUS


Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI