LOWASAAMCHANA MTULIA
Lowassa amesema hayo leo Januari 27, 2018 akiwa katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa marudio katika jimbo la Kinondoni ambapo leo maelfu ya wananchi wa Kinondoni wameweza kuwasikiliza viongozi mbalimbali wa CHADEMA kwa hoja na sera mbalimbali kuelekea uchaguzi huo ambao unatarajiwa kufanyika Februari 17, 2018.
"Kwanza nawashauri huyu Mtulia msimseme seme sana wanini huyu, mtu hovyo kabisa huyu mnampa kichwa tu sasa mtu hovyo hapaswi kuchukua muda wenu kumjadili bali nachotaka tushughulike kuwaelimisha wananchi wa Kinondoni kwanini wanastahili kutupa sisi kura, habari ya huyu bwana tuachane naye, hawa CCM hawaeleweki kule Moshi na Korogwe tulishinda lakini wakaja kusema tumeshindwa hivyo nataka kusema saizi tujiandae kulinda kura zetu" alisema Lowassa
Mbali na hilo Lowassa alimnadi Salum Mwalimu kwa kusema kuwa ni kijana safi ambaye anastahili kwenda Bungeni kuwasemea wananchi wa Kinondoni
Comments
Post a Comment