Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi aendelea kusota lumande
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Mbeya Michael Mteite, baada ya kutupilia mbali pingamizi lililowekwa siku ya jana (Jumanne) na kuweza kusikiliza ushahidi huo wa sauti kwa takribani dakika 39 uliyotolewa na shahidi namba tano wa kesi hiyo Afande Joramu Magova ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama katika Ofisi ya Upelelezi Mkoani humo.
Kutokana na hilo Wakili Mkuu wa Serikali Joseph Pande, ameieleza Mahakama kuwa wameamua kufunga ushahidi upande wa Jamhuri kwa kuwa hawaoni sababu ya kuendelea na mashahidi wengine mara baada ya kuridhika na shahidi namba tano wa Afande Joramu Magova, ambaye alikuwepo kwenye mkutano na kurekodi sauti kwa kutumia kinasa sauti.
Hata hivyo Wakili wa utetezi ukiongozwa na Boniface Mwabukusi akaiomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi siku ya Alhamisi (kesho) saa nne asubuhi kwa madai ya kuongea na wateja wake ambao wanatokea mahabusu na kuongeza kuwa upande wa utetezi utakuwa na mashahidi saba na vielelezo nane na kuiomba Mahakama shauri la mashtaka walipate pamoja na sauti za watuhumiwa ili kujipanga na wateja wake.
Kwa upande mwingine katika kesi hiyo leo imeweza kusikilizwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman A. Mbowe akiwa ameongoza na Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mbeya Sophia H. Mwakagenda ambapo nje ya Mahakama Mbowe aliwataka wanachama kuwa wavumilivu wakati kesi hiyo ikiendelea.
Comments
Post a Comment