Chadema ya mshitaki mkuu wa wilaya
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepanga leo kupeleka mashataka yake katika Kamati ya Maadili kumshataki Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu ambaye alishiriki kufanya kampeni kumnadi mgombea wa CCM jimbo la Siha.
Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amethibitisha hilo na kusema kuwa leo majira ya saa tano asubuhi watafikisha mashtaka yao kwenye Tume ya Maadili kama ambavyo wameshautiwa na Tume ya Uchaguzi (NEC).
"Tunapeleka mashtaka leo kwenye kamati ya maadili, tulipanga kupeleka saa tano asubuhi kwa hiyo mashtaka yatakwenda muda huu kumshtaki rasmi Mkuu wa Wilaya" alisema Mrema
Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu alipanda jukwaani kumnadi mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Siha, Dk Godwin Mollel, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu kwani Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa mikoa na Wakurugenzi hawapashi kushiriki katika masuala ya siasa, na hii imetokea ikiwa tayari Tume ya Uchaguzi ilishatoa onyo kwa viongozi hao kutothubutu kushiriki katika masuala ya siasa.
Comments
Post a Comment