Rais Museveni wa Uganda asema anamkubali sana Trump

KAMPALA:

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema anampenda rais wa Marekani Donald Trump katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa bunge la Afrika Mashariki jijini Kampala.

Pongezi hizo za museven kwa Trump zinakuja saa chache tuu baada ya balozi wa Uganda kwa Marekani Deborah Malac kumkosoa Trump.

Maoni hayo ya rais Museveni ni tofauti sana na viongozi wengi wanaochukizwa na kauli za Trump.

Mapema mwezi huu Trump alidaiwa kutoa kauli za kejeli juu ya nchi za Afrika wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya wahamiaji.

Trump ameyakanusha madai hayo lakini seneta mmoja aliyehudhuria mkutano huo amesema kuwa Trump alitamka maneno ya kejeli na matusi kwa nchi kama Haiti, elsalvador na nchi za Afrika.


Source BBC

Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI