Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mkoani Katavi la kiri kushindwa kuitoa miili ya wachimbaji walio fukiwa na kifusi mgodini.
Mwandishi wa habari Alinanuswe Edward akiwa katika eneo lililo karibu na shimo(Longbase) lilibomoka na kuwafukia wachimbaji wawili mmoja wapo akifahamika kwa jina la Azam Lawrence Nyembeke |
MPANDA:
Miili ya vijana wawili
waliofunikwa na kifusi cha udongo katika machimbo ya dhahabu yaliyo kijiji cha
Ibindi Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi
bado haijaopolewa kwa wiki ya pili sasa.
Mpanda radio imefika
katika eneo la Kwa Songoro lililopo kijiji cha Ibindi na kuzungumza na baadhi
ya mashuhuda wa ajali hiyo ambao wameelea kusikitishwa na tukio hilo.
Kwa mujibu wa mashahidi
wameiambia Mpanda radio kuwa mmoja ya
vijana waliopoteza maisha Azam Lawrence Nyembeke mkazi wa Iringa ndugu zake hawana taarifa mpaka sasa.
Viza ya dharura ambayo alikuwa a akiitumia marehemu Azam Lawrence Nyembeke |
Licha ya juhudi
mbalimbali zilizofanywa na wachimbaji wakishirikiana na wananchi wa eneo hilo
Jeshi la zimamoto na Uokoji mkoani katavi limekiri kushindwa kutoa miili hiyo
kwa madai ya ukosefu wa vifaa kazi
vinavyowezesha kurahisisha uokoaji huo.
Uchimbaji wa madini ni
moja kati ya shughuli ianyowakusanya vijana kutoka mikoa mbali nchini lakini
wakiwa katika hatari kubwa ya kupoteza maisha kutokana na teknolojia duni ya
uchimbaji.
Source Haruna Juma
Comments
Post a Comment