Posts

Showing posts from December, 2017

CCM ni mimi na hatujawahi kutoa kauli hiyo, huyo Mwenyekiti maadamu hakuna mwingine anayefaa kuliko yeye aendelee tu miaka 100"

Image
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amefunguka na kusema wao CCM hawajawahi kuzungumzia juu ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kushikilia nafasi hiyo kwa muda mrefu bila kufanya mabadiliko. Polepole amesema hayo wakati akimjibu moja ya mwananchi ambaye alitaka kufahamu kuwa ni kwanini Wanachama wa CCM wao ndiyo wamekuwa wakipiga sana kelele juu ya nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, ndipo hapo alipofunguka na kusema hawajawahi kuzungumzia hilo na kwa kuwa hakuna mwengine ambaye wanaona anafaa basi aendelee Mbowe kwa miaka 100. "Msemaji wa CCM ni mimi na hatujawahi kutoa kauli hiyo, huyo Mwenyekiti maadamu hakuna mwingine anayefaa kuliko yeye aendelee tu miaka 100"  aliandika Polepole  Mbali na hilo Polepole ameulalamikia upinzani wa Tanzania kwa sasa na kusema umekuwa wa kupinga kila kitu hata kwa mambo mazuri wenyewe umekuwa ukipinga tu hivyo amefananisha kuwa huenda hiyo ni siasa m...

Rais wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila ameidhinisha muswada wa marekebisho ya sheria ya uchaguzi, baada ya bunge na baraza la Seneti kutofautiana kuhusu yaliomo katika sheria hiyo.

Image
Hatimae Rais wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila ameidhinisha muswada wa marekebisho ya sheria ya uchaguzi, baada ya bunge na baraza la Seneti kutofautiana kuhusu yaliomo katika sheria hiyo. Serikali inasemasheria hiyo mpya imekuja kutatua matatizo yaliojitokeza katika chaguzi zilizopita hususan kumaliza hali ya wabunge kuchaguliwa kwa kura chache. Mbunge wa bunge la kitaifa sasa itabidi awe na asilimia moja ya wawakilishi ya kura zote alizopata. Upinzani nchini humo unasema hatua hiyo itawanyima haki wagombea binafasi na kuwaondoa kabisa katika mchakato wa uchaguzi , kwa mujibu wa Christophe Lutundula mwenyekiti wa chama cha muungano kwa ajili ya maendeleo ambae pia ni naibu mwenyekiti wa muungano wa upinzani G7. Msemaji wa muungano wa vyama vinavyomuunga mkono rais Joseph Kabila (Majorite Presidentielle) André-Alain Atundi amepongeza hatua hiyo. Mbali na sheria hiyo ya uchaguzi, rais Joseph Kabila ameidhinisha pia sheria ya bajeti ya mwaka ...

TUNDULISU ASIMAMA KWA MARA YA KWANZA TANGU KUPIGWA RISASI NA WATU WASIO JULIKANA

Image
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa katika Hospitali ya Nairobi Kenya baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana, ameanza kusimama kwa mara ya kwanza kwa msaada wa madaktari. Taarifa kutoka Hospitali ya Nairobi imeeleza kuwa Lissu kwa mara ya kwanza ameweza kusimama kwa msaada wa Physiotherapist tangu  Septemba 7, mwaka huu alipopigwa risasi mjini Dodoma, hatua chache kabla ya kufika nyumbani kwake. Akizungumza kutoka Hospitalini hapo, Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanansheria Tanganyika (TLS), amesema " Wapendwa wote wiki iliyopita niliwataarifu kwamba  madaktari wangu wamesema nitasimama, nitatembea na nitarudi Tanzania " " Leo Boxing Day nimeweza kusimama kwa mguu mmoja kwa msaada wa mababa cheza kama inavyoonekana, hatua inayofuata nitawajulisheni, " Lissu

Serikali kuanza kuwashughulikia wavaa utupu

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amesema wizara imeanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli juu ya baadhi ya wasanii ambao wanadaiwa kuwa chanzo cha kuporomoka kwa maadili ya kitanzania. Waziri Mwakyembe ametoa taarifa hiyo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari na kusema kwamba kitendo cha Rasi Magufuli kusema suala hilo, kimewapa nguvu ya kuzidi kupambana na wasanii, ambapo hapo awali walikuwa wakiwagusa huwajia juu na kulalamika. "Pale tunapoona kuna ukwiukwaji, tufumbe macho tusijali malalamiko yanavyokuja kutolewa, maana ukiwagusa wasanii walikuwa wanakuja juu sana, lakini tunashukuru mkuu wa nchi kulisemea hilo, basi na sisi tumeongezewa nguvu basi hatutaachia suala hilo kuendelea kuharibu vizazi vyetu", amesema Waziri Mwakyembe. Hivi karibuni Rais Magufuli alizitaka mamlaka husika kuwachukulia hatua wasanii wanaovaa nusu utupu kwenye kazi zao za sanaa ambazo zingine huonyeshwa kwenye ...

Miss Tanzania 2017, yafutwa

Image
Waandaji wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, Kampuni ya Lino International Agency Limited,  wamesema  kwamba hakutakuwa na Fainali za Taifa za shindano la Miss Tanzania kwa mwaka 2017. Katika taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo leo imeeleza kuwa  sababu kubwa ya kuahirishwa kwa shindano hilo ni ukosefu wa Wadhamini ambao kwa njia moja au nyingine huwezesha kufanyika kwa mashindano hayo kwa kulipa gharama mbalimbali ikiwemo zawadi za washiriki. Aidha waandaaji hao pia wamesema kuwa kuchelewa kupata kibali cha kuanza mchakato wa Miss Tanzania 2017, ambacho kilitolewa na BASATA mwezi Septemba mwaka huu pia kimechangia kukosa kwasababu muda ulikuwa umeshaenda. Mashindano ya kutafuta warembo wa Miss Tanzania yamekuwa yakifanyika kila mwaka na baadae  kuibua mastaa mbalimbali kama Wema Sepetu, Lulu Diva, Jokate Mwegelo na wengine wengi.  

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema uwepo wa uchumi imara na unaokua kwa kasi ni miongoni mwa vigezo vinavyochangia ukuaji wa haraka wa sekta ya fedha nchini.

Image
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema uwepo wa uchumi imara na unaokua kwa kasi ni miongoni mwa vigezo vinavyochangia ukuaji wa haraka wa sekta ya fedha nchini. Mh. Majaliwa ametoa kauli hiyo leo mchana wakati akizindua Mpango wa Pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Jijini Dar es Salaam. Mpango huo unatarajiwa kutekelezwa kuanzia mwaka 2018 hadi 2022. “Uwepo wa uchumi imara, miundombinu muhimu iliyojengwa na inayojengwa na Serikali pamoja na sekta binafsi, katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya vijijini, na ongezeko la watumiaji wa mitandao ya simu na huduma za mawasiliano ni kati ya fursa nzuri inayochangia ukuaji wa sekta ya fedha”, amesema Majaliwa.   Waziri Mkuu Majaliwa amesema ameupitia mpango huo na kubaini kuwa umeainisha changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi hii katika harakati zake za kuongeza matumizi ya huduma za kifedha. Katika hatua n...

Polisi wanachukulia 'serious' shambulio la Lissu.

Image
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), amefunguka na kusema wao wanaendelea na upelelezi juu ya taarifa ya kutekwa kwa Ben Saanane na kudai hawawezi kusema kila hatua wanayochukua pia amedai polisi wanachukulia 'serious' shambulio la Lissu DCI Boaz amesema hayo leo Disemba 20, 2017 wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa amepata taarifa juu ya kupotea kwa mwandishi wa habari Azory Gwanda, Ben Saanane na kudai hawawezi kuwa wanatoa taarifa kwa kila hatua ambayo wamefikia.  "Tumepata taarifa za huyo mwandishi kupotea na kwa taratibu zetu tunachukua kila hatua inayostahili kuchukuliwa wakati wa utafutaji wa mtu aliyepotea zipo taratibu ambazo tunapaswa kuzichukua sisi kama polisi, suala la Ben Sanane tumeshalisema sana sisi kama upepelezi hatuwezi kusema kila hatua tunayochukua hairuhusiwa kisheria na katika kanuni zetu za upelelezi lakini niwathibitishie kwamba kila hatua inayostahili kufanywa ili kutrace mtu ...

WANANCHI WA MJIA JUU MBUNGE WA CUF ALIYE HAMIA CCM

Image
Baadhi ya wananchi wamemjia juu na kumpa maneno ya hovyo aliyekuwa mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CUF, Maulid Mtulia ambaye amehamia CCM baada ya Mtulia kutangaza nia yake ya kutaka kugombea tena Ubunge jimbo la Kinondoni kupitia CCM Mtulia leo kupitia mtandao wake wa kijamii amesema kuwa anawapenda sana watu wa Kinondoni na kusema yupo tayari kuwatumikia tena kwa kuwapa maendeleo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)   "Kwaza, nawasalimu wote na khasa wananchi wenzangu wa jimbo la Kinondoni. Nawapa pole sana kwa maumivu makali mliyoyapata kutokana na uamuzi wangu wa kujiuzulu ubunge wa jimbo letu la Kinondoni kupitia chama cha CUF. Nawahakikishia kwamba bado nawapenda sana na niko tayari kuwatumikia tena kwa lengo la kuleta Maendeleo kwenye jimbo letu"  aliandika Mtulia  Mtulia alitumia nafasi hiyo kutangaza nia yake kutaka kugombea " Nichukie fursa hii kutangaza nia kwa wanakinondoni wote na Watanzania kwa ujumla kuwa nitachu...

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya kupitia NASA, Raila Omolo Odinga, amesema yupo tayari kufa ikiwa ndiyo gharama atakayolipa baada ya kuapishwa kama rais wa wananchi, lakini lazima haki itendeke.

Image
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya kupitia NASA, Raila Omolo Odinga, amesema yupo tayari kufa ikiwa ndiyo gharama atakayolipa baada ya kuapishwa kama rais wa wananchi, lakini lazima haki itendeke. Raila Odinga ametoa kauli hiyo alipokuwa kwenye mazishi ya Mbunge wa nchi hiyo Francis Nyenze katika eneo la Kitui, na kueleza kwamba ataapishwa kuwa rais hata kama itamgharimu hukumu ya kifo kwa kufanya hivyo. "Iwapo kifo ndio gharama ambayo lazima tuilipe kwa haki ya uchaguzi Kenya, na kwamba hakutakuwa na dhuluma za uchaguzi tena baadaye, tupo tayari kulipa hiyo gharama, tutaapishwa na wafanye kile wanataka kufanya", alisikika Raila Odinga. Odinga aliendelea kwa kusema kwamba alishinda uchaguzi wa Agosti 2017 ambao ulifutwa na Mahakama ya Juu, na kuapa kuendelea kupambana kuleta mabadiliko katika uongozi wa nchi. "Tulisema tulishindauchaguzi na tutaapishwa, tumeonywa kwa hukumu na kifo, nataka nimwambie Githu Muigai (Mwanasheria ...

Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe amtaka CAG kuchunguza ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Chato

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe amesema kuwa fedha ambazo zimelipwa kwa mkandarasi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato na ununuzi wa ndege za Bombardier na Boeing hazikuidhinisha na CAG. Zitto Kabwe amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kuelezea Maazimio ya Kamati kuu ya ACT Wazalendo kuhusiana na mambo mbalimbali yanayoendelea nchini kwa sasa.  Ametoa ufafanuzi kuwa Utaratibu unataka fedha kuingia kwenye Mfuko Mkuu (Consolidated Fund) na kisha kuidhinishwa na CAG, na ndipo Serikali kuanza kutumia. Sanjari na hayo amefafanua kuwa Shilingi bilioni 300 kutumika na Serikali bila kushirikisha Bunge na kufuata sheria za nchi ni kusigina Katiba na kudharau Taasisi za Uwajibikaji za nchi . Aidha Kamati Kuu y a ACT Wazalendo imemtaka CAG afanye ukaguzi maalum wa fedha hizo na kutoa taarifa kwa Bunge ili sasa Bunge liweze kuiwajibisha na kuisimamia Serikali vizuri. Source Eatv Editor Alinanuswe Edward

Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania aiga CCM

Image
Aidha Mh. Dkt. Salim ameahidi kuendelea kushirikiana na kuwa mtiifu kwa Chama na Sekali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaongozwa  DODOMA Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Salim Ahmed Salim leo amewaaga Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye kikao kinachoendelea mjini Dodoma. Dkt. Salim ameaga baada ya kumaliza muda wake wa miaka mitano ya kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho.  Waziri Mkuu huyo wa zamani amempongeza Mwenyekiti wa CCM Rais John Pombe Magufuli kwa uongozi wake ambao umekiwezesha Chama kuimarika. Katika hatua nyingine Dkt. Salim amewashukuru wajumbe wote wa Kamati Kuu na viongozi wa Chama kwa ushirikiano ambao wamemwonesha muda wote wa ujumbe wake. Aidha Mh. Dkt. Salim ameahidi kuendelea kushirikiana na kuwa mtiifu kwa Chama na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaongozwa na Chama cha Mapinduzi.   na Chama cha Mapinduzi Aidha Mh. Dkt. Salim ameah...

TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania (Takukuru) inamshikilia aliyekuwa Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba

DAR – ES SALAAM. TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania (Takukuru) inamshikilia aliyekuwa Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa katika uchaguzi wa viongozi wa chama hicho. Msemaji wa Takukuru, Mussa Misalaba amesema , kwamba Mukoba amekamatwa na maofisa wa uchunguzi wa taasisi hiyo kwenye viwanja vya Chimwaga ambako uchaguzi huo ulikuwa unaendelea. Misalaba alidai kwamba Rais huyo wa zamani CWT alikuwa anajaribu kuwahonga wapiga kura. Mukoba alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa CWT mwaka 2002 na mwaka 2007 alichaguliwa kuwa Rais wa chama hicho, kabla ya mwaka 2014, kuchaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta). Na kustaafu ualimu hivi karibuni. Source EATV Editor Alinanuswe Edward.

CHADEMA MKOA WA KATAVI YATOA MSIMAMO WAKE KWANAO KIHAMA CHAMA HICHO.

Image
Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoa wa Katavi Laulent Mangweshi amewataka wanachama wa chama hicho kutoyumbishwa na baadhi ya wanasiasa ambao hujiunga na chama tawala. Akizungumza na Mpanda radio fm amesema vitendo vya wanasiasa hao ambao miongoni mwao ni kundi kubwa la madiwani mkoani Arusha na Mbunge mmoja hakuwezi kubadilisha msimamo wa chama hicho katika kuendeleza sera zake. Katika hatua nyingine amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono sera za chama hicho katika mapambano ya uwepo wa demokrasia ya kweli nchini Tanzania. Vugu vugu hilo la kisiasa linalo vikabili vyama pinzani kwa kiasi kikubwa limezua mijadala mingi miongoni mwa Jamii kwa madai kuwa ni  usariti kwa wapiga kura.  Lakini Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA Joshua Nasari alionyesha mkanda wa video ulikuwa ukionyesha madiwani wakihongwa ili kujiunga na chama cha CCM.   Source OFISI YA CHADEMA Editor Alinanuswe Edward

Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli amesema Serikali ina mpango wa kufuta mifuko ya hifadhi ya jamii na kubakiza miwili.

Image
DODOMA Rais wa Tanzania Dk John  Pombe Magufuli amesema Serikali ina mpango wa kufuta mifuko ya hifadhi ya jamii na kubakiza miwili. Amesema mifuko itakayobaki ni kwa ajili ya kuhudumia wafanyakazi wa sekta binafsi na ya umma. Rais Magufuli amesema Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) litabaki kwa ajili ya kuhudumia wafanyakazi wa sekta binafsi wakati mifuko mingine yote itaunganishwa na kuwa mmoja. Amesema hayo alipofungua mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mjini Dodoma ambapo ameeleza kuwa mifuko hiyo imegeuka dili kwa vigogo ambao huamua kujenga majumba makubwa ili wapate asilimia 10. Mifuko mingine inayotoa huduma ya hifadhi ya jamii ni PSPF, LAPF, PPF na GEPF.

Wakulima wa zao tumbaku mkoani Katavi wailaumu serikali kushindwa kutekeleza ahadi yake.

Image
Katavi Na Alinanuswe Edward. Wakulima wa zao la tumbaku wa chama cha msingi cha ushirika Mpanda Kati Mkoani Katavi wameilaumu serikali kushindwa kutekeleza agizo lake la kuhakikisha tumbaku iliyo kosa soko inanunuliwa. Wakulima hao  kwa nyakati tofauti wamesema mpaka sasa hawajui hatima ya ununuzi wa tumbaku yao huku wengine wakisema wameathirika kiuchumi na maisha kwa ujumla. Hivi karibuni,mwenyekiti chama cha msingi cha Ushirika Mpanda Kati Bw.Sosipeter Salvatory ,alisema kuna kiasi cha tani elfu ishirini na mbili ambazo hazijanunuliwa kati ya kiasi chote cha tumbaku iliyozalishwa katika msimu wa mwaka   mwaka 2016/2017. Mnamo Novemba 17 mwaka huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiahirisha vikao vya Bunge mjini Dodoma alieleza kuwepo kwa kampuni itakayo nunua Tumbaku iliyosalia pamoja na Mbaazi.

Mkoa wa Katavi umetengewa kiasi cha billion 14.392 kwaajili ya ukarabati wa barabara zenye urefu wa kilomita 68.60.

Image
KATAVI Na Alinanuswe Edward. Mkoa wa Katavi umetengewa kiasi cha billion 14.392  kwaajili ya ukarabati wa barabara zenye urefu wa kilomita 68.60. Kauli hiyo imetolewa leo Kaimu Meneja wa TANROAD Martin Mwakabende kwenye Uzinduzi wa utekelezaji wa kazi za matengenezo ya barabara ya mwakaa 2016/17 na mwaka 2017/18   katika kikao cha 10 cha Bodi ya Barabara ya mkoa wa Katavi(RRB). Aidha ameongeza kusema kuwa Wameanza kuthibiti Magari mazito barabarani kutokana na  kuwa na mizani ya kuhamishika kwa lengo la kudhibiti uharibifu wa barabara.. Mgeni rasmi katika kikao hicho ambaye ni mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Rafael Mhuga amesisitiza uwajibikaji kwa vitendo ili kufikia malengo. Katika utekelezaji wa Mradi huo wa matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2016/17 zilitengwa  sh.billioni  15.431 Na mwaka 2017/18  sh.billion 14.392 kwaajili ya ukarabati wa Barabara.

Mbunge Hussein Bashe (CCM) na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe wameungana kwa pamoja kulaani kitendo cha Serikali kuhoji uraia wa Askofu

Image
Mbunge Hussein Bashe (CCM) na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe wameungana kwa pamoja kulaani kitendo cha Serikali kuhoji uraia wa Askofu wa Jimbo la Katoliki, Rulenge Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Severine Niwemugizi. Wabunge hao kwa nyakati tofauti wameeleza hisia zao juu ya jambo hilo na kudai  watu wanaofanya jambo hili ni wazi hawana hofu ya Mungu lakini pia ni njia ya kuwatisha watu hususani wale ambao wanakuwa wanaikosoa serikali.  "Najuai inavyokuwa unapoambiwa ama kuanza kujazishwa fomu na kuhojiwa juu ya Uraia Wako ni kama kujazishwa fomu kuambiwa huyu sio Mama yako or Baba yako. Pole Askofu Severine Niwemugizi wanaofanya haya hawana hata hofu ya Mungu"  aliandika Hussein Bashe  Hata hivyo Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe naye amechangia na kusema kuwa suala la Uraia hutumika kama silaha dhidi ya watu ambao wanaonekana kuikosoa Serikali kwa mambo mbalimbali ambayo serikali inakuwa inafanya.  "Baba ...

Zaidi ya wanafunzi 9000 mkoani Katavi kukosa nafasi kutokana na uhaba wa vyumba vya madalasa

Image
KATAVI Zaidi ya wanafunzi 9000 waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mkoani Katavi wamekosa nafasi ya kuingia kidato cha kwanza kwa mwaka 2018 kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa.  Akitangaza matokeo ya mtihani huo katika kikao maalumu cha uchaguzi wa wanafunzi Afisa Elimu mkoa wa Katavi Ernest Hinju amesema jumla watahiniwa 7,190 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za kutwa. Aidha watahiniwa 162 hawakuweza kufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali hali iliyopelekea wadau wa elimu kujadili changamoto za kushuka kwa elimu, kwani kulinganisha na mwaka uliopita mkoa wa Katavi umeshika nafasi ya 9 kitaifa kutoka nafasi ya 2 mwaka uliopita  Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Katavi Bwana Gideon Marandu amezitaka halmashauri zote kuhakikisha wanafunzi waliokosa nafasi wanapata nafasi ifikapo Februari mwaka 2018

MIILI YA ASKARI 14 WALIO WA JWTZ WALIO UAWA MCHINI KONGO WALIKOKUWA WAKILINDA AMANI IMEWASILI NYUMBANI TANZANIA MUDA HUU.

Image
Miili 14 ya askari wa JWTZ waliouawa nchini Kongo walikokuwa wakilinda amani, imewasili nyumbani nchini Tanzania Alasiri hii, na ndege ya jeshi la ya Umoja wa Mataifa, kwenye uwanja wa ndege wa jeshi jijini Dar es salaam. Zoezi la kupokea miili hiyo limeongozwa na Waziri wa Ulinzi Dkt. HUssein Mwinyi, na maaskari wengine wa JWTZ ambao walishusha miili hiyo na kupiga gwaride mbele ya miili ya askari hao. Baada ya miili hiyo kupokelewa uwanja wa ndege itapelekwa katika hospitali ya jeshi ya Lugalo ili kuwapa fursa maafisa kuifanyia uchunguzi miili hiyo, kabla ya kutangazwa kwa tarehe ya mazishi. Ijumaa ya Desemba 8 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Antonio Guterres alitoa taarifa ya vifo vya askariu hao ambao walikuwa nchini Kongo kulinda amani, huku 44 wakijeruhiwa vibaya, 8 wakiwa mahututi na wawili hawajulikani waliko.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa wapalestina ni lazima wakubali kuwa Jurusalem ndio mji mkuu

Image
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa wapalestina ni lazima wakubali kuwa Jurusalem ndio mji mkuu wa Israel ili amani iweze kupatikana. Netanyahu amesema Jerusalem umekuwa mji mkuu wa Israel kwa miaka 3,000 na haujakuwa mji mku wa watu wengine. Amesema hayo huku maandamano yakiendelea kwenye ulimwengu wa kiislamu kufuatia hatua ya Marekani kuutambua Jurusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Ghasia zimezuka karibu na ubalozi wa Marekani nchini Lebanon na kwingineno siku ya Jumapili. Akiongea mjini Paris baada ya mazungumzo na rais wa Ufaransa Emmauel Macron, Bw Netanyahu amesema kuwa jitihada za kuwanyima wayahudi mji wa wa Jerusalem ni kitu kibaya.

Kheri James atangazwa kuwa Mwenyekiti mpya UVCCM

Image
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa (UVCCM), leo umemtangaza Kheri James kuwa Mwenyekiti mpya atakayeongoza kwa miaka mitano. Kheri ametangazwa mshindi baada ya kupata Kura 319 kati ya kura 583 zilizopigwa akiwashinda wenzake 6 aliokuwa akichuana nao kuwania nafasi hiyo. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imechukuliwa na Tabia Mwita. Mkutano wa Uchaguzi wa UVCCM umefanyika mjini Dodoma kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ndiye aliye simamia uchaguzi huo na kumtangaza mshindi. Mkutano huo wa uchaguzi wa UVCCM ulifunguliwa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. John Pombe Magufuli na unafungwa leo na Rais wa Zanziobar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.

Vijana mkoa wa katavi wametakiwa kuungana katika uwajibikaji ili kujiletea maendeleo

Image
Vijana mkoa wa katavi wametakiwa kuungana katika uwajibikaji ili kujiletea maendele na taifa kwa ujumla. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa  umoja wa Vijana CCM (UVCCM) mapema leo alipokuwa akizungumza na Mpanda radio fm kwa njia ya simu akiwa mjini Dodoma kuhudhuria mkutano mkuu wa chama hicho. Ameitaja shabaha kubwa kuwa ni kuwaunganisha vijana kupitia maendeleo na kwamba hii ndio itakuwa suruhu ya kuondoa migawanyiko miongoni mwao ambayo hushudiwa kwa kiwango cha juu katika vipindi vya uchaguzi.  Aidha ameongeza kusema kuwa ilikufikia Tanzania ya viwanda   ni lazima vijana wote waelekeze nguvu zaidi katika Kilimo. Wakati haya yakijiri Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Dk John Pombe Magufuli ameutaka umoja wa vijana UVCCM nchini kuwa na mawazo mapya yenye tija kwa jamii na taifa.

MASHEHE WAJIUDHURU KATAVI

KATAVI MASHEHE watano akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) Mkoa wa Katavi, Shehe Shaaban Bakari wamejiuzulu uongozi wakidai kuwepo kwa migogoro ya uongozi na ukiukwaji wa Katiba ya Bakwata. Halmashauri ya baraza hilo inaundwa na viongozi sita ambao ni mashehe, watano kati yao ndio waliotangaza kujiuzulu ambao ni Mwenyekiti wao Shehe Bakari, Shehe Mashaka Kakulukulu, Shehe Hassan Mbaruku, Shehe Said Haruna Omary na Shehe Mohamed Sigulu. Wakitangaza uamuzi huo  mbele ya waandishi wa habari, Shehe Kakulukulu amesema haoni sababu ya kuendelea kuwa kiongozi wa halmashauri ya baraza hilo akidai kumekuwepo na baadhi ya mambo ya kimaendeleo ambayo hayaendi sawa. Kauli hiyo imeungwa mkono na mashehe wengine, huku Shehe Sigulu akidai kuwa msuguano uliopo wa kiuongozi ndani ya Bakwata umesababishwa na mwalimu wa madrasa katika Msikiti Mkuu mjini Mpanda kuamua kuacha kazi ya kufundisha hivi karibuni.

Muungano mkuu wa upinzani nchini Kenya NASA, umetangaza kuahirishwa kwa shughuli ya kumuapisha kinara mkuu wa muungano huo Raila Odinga na Stephen Kalonzo Musyoka, kama rais na makamu wa rais mtawalia wa Jamhuri ya Kenya.

Image
Muungano mkuu wa upinzani nchini Kenya NASA, umetangaza kuahirishwa kwa shughuli ya kumuapisha kinara mkuu wa muungano huo Raila Odinga na Stephen Kalonzo Musyoka, kama rais na makamu wa rais mtawalia wa Jamhuri ya Kenya. Shughuli hiyo ilikuwa imepangiwa kuandaliwa Jumanne tarehe 12 mwezi huu. Katika taarifa iliyotolewa leo na muungano wa NASA ni kuwa tarehe mpya ya kuapishwa kwa Bw. Odinga na Musyoka, na pia kuzinduliwa kwa mabunge ya wananchi itatangazwa baadaye. Odinga alijiondoa kwenye uchaguzi mkuu ambao ulifanyika tarehe 26 mwezi Oktoba ambapo Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi. Uchaguzi huo wa tarehe 26 ulikuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama ya juu nchini nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu. Wakati wa kuapishwa kwake tarehe 28 mwezi uliopita, Rais Uhuru Kenyatta aliahidi kuunganisha taifa katika muhula wake wa pili uongozini katika sherehe ambayo ilisusiwa na viongozi wa upinzani. Akihutubu baada ya kula ki...

Chama cha watu wenye Ualbino Tanzania (TAAS) Mkoani Katav chakemea ubaguzi dhidi ya walemavu

Na.Issack Gerald Chama cha watu wenye Ualbino Tanzania (TAAS) Mkoani Katavi kimewataka watanzania kutowaita wao kama watu wenye ulemavu wa ngozi albino badala yake wawaite watu wenye Ualbino. Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa chama hicho Mkoani Katavi Bw.Victus Kweka kupitia kikao cha kujadili kupinga ukatiri,unyanyasaji na ukandamizaji wa haki za watu wenye ulemavu kwa kuwanyima haki za msingi kama elimu,afya na haki nyingine za kibinadamu. Amesema rangi ya ngozi waliyonayo watu wenye ualbino siyo ulemavu wa ngozi bali wao wanahesabika katika kundi la watu wenye ulemavu wa macho kutokana hali waliyonayo. Kwa upande wake mratibu wa wa elimu jumuishi Wilayani Mpanda Bi.Ashura Shabaani ambaye pia ni msichana mwenye ualbino amesema mpaka sasa bado kuna baadhi ya watu wenye ualbino wanaojinyanyapaa. Amewataka watu wenye ualbino kuchanganyikana na jamii ili kupata elimu inayowawezesha kufahamu haki zao,kupatiwa mafuta ya kupunguza mionzi mikali ya jua. Watu wenye ualbino...

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, John Pombe Magufuli ametaka kuvunjwa kwa bodi ya wadhamini ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, John Pombe Magufuli ametaka kuvunjwa kwa bodi ya wadhamini ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM na kuwataka viongozi watakaochaguliwa kuhakiki miradi yote ya umoja huo kuanzia ngazi ya chini. Akifungua Mkutano wa tisa wa Jumuia hiyo ambao ajenda yake kuu ni kufanya uchaguzi wa viongozi, Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye pia ni Rais wa Tanzania, amesema kuwa miradi ya UVCCM mapato yake yamekuwa hayajulikani yanapoenda hivyo inahitaji kuhakikiwa na kuwekwa pamoja ili kuweza kuleta tija kwa umoja huo huku akisema bodi ya wadhamini imekuwa haina msaada katika jumuia hiyo. Rais Magufuli pia amewataka UVCCM kuchagua viongozi wanaofaa na wanaoichukia rushwa ili waweze kuisaidia serikali badala ya kuwa viongozi wa kuyumbishwa na misimamo ya watu wenye pesa hali iliyofanya umoja huo kukosa muelekeo hasa kipindi cha uchanguzi. Katika mkutano huo wanachama wapya waliojiunga na chama hicho hivi karibuni k...