CHADEMA MKOA WA KATAVI YATOA MSIMAMO WAKE KWANAO KIHAMA CHAMA HICHO.
Mwenyekiti wa Chama cha
demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoa wa Katavi Laulent Mangweshi amewataka
wanachama wa chama hicho kutoyumbishwa na baadhi ya wanasiasa ambao hujiunga na
chama tawala.
Akizungumza na Mpanda radio fm amesema vitendo vya wanasiasa
hao ambao miongoni mwao ni kundi kubwa la madiwani mkoani Arusha na Mbunge
mmoja hakuwezi kubadilisha msimamo wa chama hicho katika kuendeleza sera zake.
Katika hatua nyingine amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono sera za chama hicho katika mapambano ya uwepo wa demokrasia ya kweli nchini Tanzania.
Vugu vugu hilo la kisiasa linalo vikabili vyama pinzani kwa
kiasi kikubwa limezua mijadala mingi miongoni mwa Jamii kwa madai kuwa ni usariti kwa wapiga kura.
Lakini Mbunge wa
Arusha Mjini kupitia CHADEMA Joshua Nasari alionyesha mkanda wa video ulikuwa
ukionyesha madiwani wakihongwa ili kujiunga na chama cha CCM.
Source OFISI YA CHADEMA
Editor Alinanuswe Edward
Comments
Post a Comment