Chama cha watu wenye Ualbino Tanzania (TAAS) Mkoani Katav chakemea ubaguzi dhidi ya walemavu
Na.Issack Gerald
Chama cha watu wenye Ualbino Tanzania
(TAAS) Mkoani Katavi kimewataka watanzania kutowaita wao kama watu wenye
ulemavu wa ngozi albino badala yake wawaite watu wenye Ualbino.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa
chama hicho Mkoani Katavi Bw.Victus Kweka kupitia kikao cha kujadili kupinga
ukatiri,unyanyasaji na ukandamizaji wa haki za watu wenye ulemavu kwa kuwanyima
haki za msingi kama elimu,afya na haki nyingine za kibinadamu.
Amesema rangi ya ngozi waliyonayo
watu wenye ualbino siyo ulemavu wa ngozi bali wao wanahesabika katika kundi la
watu wenye ulemavu wa macho kutokana hali waliyonayo.
Kwa upande wake mratibu wa wa elimu
jumuishi Wilayani Mpanda Bi.Ashura Shabaani ambaye pia ni msichana mwenye
ualbino amesema mpaka sasa bado kuna baadhi ya watu wenye ualbino
wanaojinyanyapaa.
Amewataka watu wenye ualbino kuchanganyikana
na jamii ili kupata elimu inayowawezesha kufahamu haki zao,kupatiwa mafuta ya
kupunguza mionzi mikali ya jua.
Watu wenye ualbino Tanzania wamekuwa hawachangamani
na jamii wakiogopa mauaji dhidi yao kama ilivyokuwa katika miaka michache
iliyopita.
Comments
Post a Comment