Mbunge Hussein Bashe (CCM) na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe wameungana kwa pamoja kulaani kitendo cha Serikali kuhoji uraia wa Askofu



Mbunge Hussein Bashe (CCM) na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe wameungana kwa pamoja kulaani kitendo cha Serikali kuhoji uraia wa Askofu wa Jimbo la Katoliki, Rulenge Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Severine Niwemugizi.
Wabunge hao kwa nyakati tofauti wameeleza hisia zao juu ya jambo hilo na kudai  watu wanaofanya jambo hili ni wazi hawana hofu ya Mungu lakini pia ni njia ya kuwatisha watu hususani wale ambao wanakuwa wanaikosoa serikali. 
"Najuai inavyokuwa unapoambiwa ama kuanza kujazishwa fomu na kuhojiwa juu ya Uraia Wako ni kama kujazishwa fomu kuambiwa huyu sio Mama yako or Baba yako. Pole Askofu Severine Niwemugizi wanaofanya haya hawana hata hofu ya Mungu" aliandika Hussein Bashe 
Hata hivyo Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe naye amechangia na kusema kuwa suala la Uraia hutumika kama silaha dhidi ya watu ambao wanaonekana kuikosoa Serikali kwa mambo mbalimbali ambayo serikali inakuwa inafanya. 
"Baba askofu pole sana. Kuna watu wakubwa tu kwenye Taasisi nyeti wanaamini kwa ushahidi kuwa aliyeagiza uhojiwe mwenyewe sio raia wa Tanzania. Suala la Uraia hutumika kama silaha dhidi ya wakosoaji wa Serikali. Ni ushamba" alisisitiza Zitto Kabwe 
Askofu Severine Niwemugizi amesema kuwa amehojiwa kuhusu uraia wake mara mbili. Mara ya kwanza aliitwa kwenye ofisi za uhamiaji Ngara Novemba 28, 2017 na mara ya pili Disemba 4, 2017.

Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI