Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania aiga CCM
Aidha Mh. Dkt. Salim ameahidi kuendelea kushirikiana
na kuwa mtiifu kwa Chama na Sekali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo
inaongozwa
DODOMA
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. Salim Ahmed Salim leo amewaaga Wajumbe wa Kamati
Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye kikao kinachoendelea mjini Dodoma.
Dkt. Salim ameaga baada ya kumaliza muda
wake wa miaka mitano ya kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho.
Waziri Mkuu huyo wa zamani amempongeza
Mwenyekiti wa CCM Rais John Pombe Magufuli kwa uongozi wake ambao umekiwezesha
Chama kuimarika.
Katika hatua nyingine Dkt. Salim
amewashukuru wajumbe wote wa Kamati Kuu na viongozi wa Chama kwa ushirikiano ambao
wamemwonesha muda wote wa ujumbe wake.
Aidha Mh. Dkt. Salim ameahidi kuendelea
kushirikiana na kuwa mtiifu kwa Chama na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambayo inaongozwa na Chama cha Mapinduzi.
Comments
Post a Comment