Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, John Pombe Magufuli ametaka kuvunjwa kwa bodi ya wadhamini ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM
Akifungua Mkutano wa tisa wa Jumuia hiyo ambao ajenda yake kuu ni kufanya uchaguzi wa viongozi, Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye pia ni Rais wa Tanzania, amesema kuwa miradi ya UVCCM mapato yake yamekuwa hayajulikani yanapoenda hivyo inahitaji kuhakikiwa na kuwekwa pamoja ili kuweza kuleta tija kwa umoja huo huku akisema bodi ya wadhamini imekuwa haina msaada katika jumuia hiyo.
Rais Magufuli pia amewataka UVCCM kuchagua viongozi wanaofaa na wanaoichukia rushwa ili waweze kuisaidia serikali badala ya kuwa viongozi wa kuyumbishwa na misimamo ya watu wenye pesa hali iliyofanya umoja huo kukosa muelekeo hasa kipindi cha uchanguzi.
Katika mkutano huo wanachama wapya waliojiunga na chama hicho hivi karibuni kutoka vyama mbalimbali vya upinzani waliwataka vijana wa CCM kuwa mstari wa mbele kuisaidia serikali.
Comments
Post a Comment